Wafanyabiashara
wa mbolea nchini wametakiwa kuuza bidhaa hiyo kwa kufuata bei elekezi
zilizotangazwa na Waziri wa Kilimo na Mifugo Dkt. Charles Tizeba , kwani
lengo la serikali ni kuhakikisha wakulima wanapata mbolea ya uhakika na
kwa be nafuu.
Agizo
hilo limetolewa jana Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea TFRA Bw. Lazaro Kitandu, katika mahojiano
aliyoyafanya na vyombo vya habari, kufuatia taarifa za kuwepo kwa
wafanyabiashra wachache wanaotaka kuvuruga nia hiyo nzuri ya serikali
kwa kuanza ulanguzi wa mbolea
Aidha,
Bw. Kitandu alitaja sababu ya kuwa na bei elekezi ya mbolea kuwa ni
kukuza kilimo na kuongeza mavuno ya mazao ambayo ndio malighafi kuu
inayohitajika wakati huu ambapo serikali inatekeleza mipango ya ukuaji
wa viwanda, kama msingi mkuu wa kufikia malengo ya kuwa taifa la uchumi
wa kati ifikapo mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment