Mwalimu
wa madrasa, Abdillah Sharifu, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela
baada ya kutiwa hatiani kwa kumlawiti mtoto wa kiume wa miaka 11.
Mshtakiwa
anadaiwa kumlawiti mtoto huyo na pia kumtishia kuwa angemroga endapo
angetoa taarifa kwa wazazi wake kuwa anamfanyia kitendo hicho.
Akisoma hukumu, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Hassan amesema ameridhishwa na ushahidi wa mashahidi wanne akiwemo daktari.
“Mshtakiwa
nimekutia hatiani kama ulivyoshtakiwa, ninakuhukumu kifungo cha miaka
30 jela ili iwe fundisho kwako na watu wengine wenye tabia mbaya kama
hii,” amesema.
Hakimu Hassan amesema kitendo kilichofanywa na mshtakiwa ambaye ni mwalimu wa dini ni cha kikatili.
Shahidi
huyo aliieleza Mahakama kuwa mshtakiwa alimfanyia ukatili huo, huku
akimtishia kuwa iwapo angethubutu kutoa siri hiyo angemroga.
“Mara
kwa mara alikuwa akinifanyia mchezo huu hadi nilipomwambia mama na
kisha kwenda kufungua kesi katika kituo cha polisi Mazizini,” alisema
mtoto huyo katika ushahidi alioutoa mahakamani.
Katika
ushahidi wa mama mzazi wa mtoto huyo, alidai baada ya kuripoti polisi
walikwenda hospitali ambako kwa mujibu wa vipimo vya daktari licha ya
kutokuwa na michubuko ilionekana aliingiliwa.
Mshtakiwa
alidai ana mke kipofu na kwamba, hafanyi vitendo hivyo isipokuwa
alikuwa na ugomvi na mama wa mtoto huyo na ndiyo sababu ya kumfungulia
kesi.
Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kuifafanulia Mahakama chanzo cha ugomvi hivyo ilitupilia mbali utetezi wake na kumtia hatiani.
Mshtakiwa alitenda kosa hilo, Februari 25 katika eneo la Moshi Bar, Gongo la Mboto.
No comments:
Post a Comment