Mama Mwenye nyumba Bi,Scolastica Nicodemo akizungumza na mmmoja wa viongozi wa dini waliofika kushuhudia mzoga huo
Wananchi wakishangaa
Viongozi wa dini wakiteketeza vitu pamoja na mzoga huo ambao umekutwa kwenye nyumba hiyo.
Wananchi wakiendela kushangaa tukio hilo
*****
Katika
hali isiyo ya kawaida wananchi wa Mtaa wa 14 Kambarage Kata ya
Buhalahala Wilaya na Mkoa wa Geita wamepigwa butwaa baada ya kukuta
mzoga wa kuku ukiwa umevishwa sanda kwenye familia ya Emmanuel
Kabodi.
Mama
wa familia hiyo Bi Scolastica Nicodemo ameelezea kuwa wakati
akifanya usafi aliona kuna kitu kimefungwa na shuka jeupe nyuma ya geti na alipojaribu kukiangalia aligundua ni sanda imefungwa kuku na ndipo walipofanya maamuzi ya kumwita mchungaji kuja kujionea.
Askofu
wa kanisa la TMRC Mkoani Geita Stephano Saguda ameiasa jamii kuachana
na masuala yanasosadikiwa kuwa ni ya kishirikina kwani vitendo hivyo
havimpendezi Mungu na havikubaliki kwenye jamii ya watanzania .
Mjumbe
wa Mtaa Huo Stephano Mayovu Matata amesema hii ni mara ya pili kutokea
kwa tukio hilo kwani mara ya kwanza lilitokea tukio la kufukuliwa kwa
mtoto na kwamba ni vyema kwa mtu ambaye anafanya vitendo hivyo kuachana
navyo mara moja kwani wakimbaini mtu wa namna hiyo hawataweza
kumvumilia.
Wananchi waliokuwa wamekusanyika katika eneo hilo wamesikitishwa na kitendo hicho kinachohusishwa na imani za kishirikina.
Mtaa
wa 14 Kambarage umeendelea kukumbwa na vitendo vinavyosadikiwa ni vya
imani za kishirikiana vya mara kwa mara na kusababisha hofu kubwa kwa
watu ambao wanaishi maeneo hayo.
Imeandaliwa na Joel Maduka
No comments:
Post a Comment