Tuesday 8 October 2013

MWENGE WA UHURU WAMALIZA KUKIMBIZWA JIJINI MBEYA AMBAPO JUMLA YA MIRADI 9 IMEZINDULIWA YENYE THAMANI YA SHILINGI 4,741,271,715

Mwenge wa Uhuru ukiwasili Jijini Mbeya katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Iwambi  ukitokea Wilaya ya Chunya ulikomaliza mbio zake  ukiwa umebebwa na wakimbiza mwenge kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akisoma taarifa ya  Mbio za Mwenge ulivyokimbizwa Wilayani kwake kabla ya kumkabidhi mkuu wa Wilaya ya Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla King akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa  Juma Ali Simai pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mbeya wakisubiri kukabidhiwa Mwenge wa Uhuru kutoka Wilayani Chunya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Deodatus Kinawiro akitamka kiapo cha kumkabidhi Mwenge pamoja na Wakimbiza Mwenge wa Kimkoa na Kitaifa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla King.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla King akipokea Mwenge kutoka kwa Mkuu wa wilaya ya Chunya tayari kwa kuanza kuukimbiza katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Iwambi wakisoma Shairi wakati mwenge ukiweka Jiwe la msingi katika jengo la utawala la shule hiyo pamoja na kuona  klabu za kupambana na rushwa shuleni hapo.
Vituko na vichekesho vilikuwa mbele katika kupamba shughuli za Mwenge katika jiji la Mbeya.
Mradi wa ujenzi wa daraja ulifunguliwa katika kata ya Itende 
Wananchi wa Jiji la Mbeya pamoja na Wanafunzi waliojitokeza kuupokea Mwenge wakiushika kwa karibu kama ishara ya kuutukuza Utanzania  
Nyumba ya Watumishi wa Zahanati ya Mwansekwa iliyopo katika kata ya Mwansekwa ilifunguliwa.
Mradi wa maji katika kata ya Itagano uliwekewa jiwe la msingi mradi unaotarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi wa Novemba.
Mwenge wa Uhuru pia ulizindua Ushirika wa wasafirishaji wa Bajaji Jiji la Mbeya katika ofisi zao zilizopo katika kata ya Iganzo. 
Mwenyekiti wa Ushirika wa Wasafirishaji wa Bajaji Mbeya Idd Ramadhani akionesha Hati ya Utendaji bora waliyotunukiwa na kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa. 
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Ali Simai pamoja na mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dr. Norman Sigalla King wakipandikiza miche ya miti ya mbao baada ya Mwenge kutembelea na kuona na kushiriki uoteshaji wa miche na bustani ya Bright Future Charity iliyopo Block T.
Christopher Emmanuel Mkimbiza mwenge wa Uhuru akitoa salamu na ujumbe wa mwenge kwa mwaka 2013 katika viwanja vya Shule ya Msingi RuandaNzovwe ambapo Mwenge unakesha kabla ya kuelekea Wilayani Mbarali baada ya kumaliza ziara yake Jijini mbeya
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya Musa Zungiza pamoja na viongozi wengine wakifuatilia kwa makini shughuli zinazoendelea uwanjani hapo.

No comments: