Tuesday, 31 May 2016

Wabunge wa Upinzani wametoka nje ya bunge kuonyesha kutokuwa na imani na Naibu Spika Tulia Ackson

Wabunge wa vyama vya upinzani leo wametoka nje kwa mara nyingine kupinga Naibu Spika Dk. Tulia Acksonkuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.

Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.

Hata hivyo Dk. Tulia ameanza kupaniwa na wapinzani tangu jana. Ni kwa madai kuwa wapinzani hawamwamini tena.

Wameeleza kuwa, namna anavyoliongoza Bunge, kauli zake na kuyumba kwake katika kusimamia haki kwa wabunge wa Ukawa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumechochea kuonekana kuwa, nafasi aliyonayo haimstahili.

Kutokana na hali hiyo, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana aliahidi kuanzisha mgomo dhidi ya Dk. Tulia.

Mbowe aliwaambia hayo wabunge wenzake mjini Dodoma kwenye kikao cha dharura alichoitisha na kushirikisha waandishi wa habari.

Alisema, Dk. Tulia ndio tatizo kuu la Bunge la Kumi na Moja na kwamba, kiongozi huyo wa Bunge kila anapokuwa kwenye kiti na kuongoza Bunge, mtafaruku hutokea.

“Nitapendekeza kuwa kila kikao cha Bunge kinachoongozwa na Tulia Ackson, sote tutoke nje ili kuonesha kwamba hatuna imani naye katika kuendesha shuguli za bunge,” Mbowe alisema jana.

Utekelezwaji wa kauli ya Mbowe umeanza leo ambapo sasa Dk. Tulia amebaki na wabunge wa CCM pekee.

Monday, 30 May 2016

Bunge Lawasimamisha Wabunge 7 Kwa Kufanya Vurugu Bungeni


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge limepitisha azimio la  kuwasimamisha kuhudhuria vikao vya Bunge baadhi ya wabunge wa Kambi ya Upinzani waliohusika katika kufanya vitendo vya vurugu ndani ya ukumbi na kudharau Mamlaka ya Spika Januari, 27, 2016.

Wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao hivyo ni Mhe.Kabwe Zubeiri Ruyangwa Kabwe, Mhe.John Heche, Mhe.Halima Mdee,Mhe.Tundu Lissu, Mhe.Halima Mdee, Mhe.Pauline Gekul  na Mhe. Ester Bulaya.

 

 Azimio la adhabu kwa wabunge hao limetolewa na Bunge chini ya Kifungu cha 30A (1) cha sheria ya Haki Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na kanuni ya 74 (4) na (6).

Akisoma adhabu hizo Mwenyekiti wa kamati hiyo yenye wajumbe 15 Mhe.George Huruma Mkuchika amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na Kamati hiyo kwa kuwaita na kuwahoji wahusika ulibaini kuwa wabunge hao walitenda kosa kwa kukiuka kanuni zinazoliongoza bunge hilo.

 

 Imebainishwa kuwa Mhe.Zitto Kabwe alivunja masharti ya Kifungu cha 24(c), (d) na (e) cha Sheria ya Haki na Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na Kanuni ya 60(2) na (12) , 74(1) na (b) kwa kusimama na kuzungumza bila kufuata utaratibu na kudharau mamlaka ya Spika.

Kamati hiyo ilibaini kuwa Mhe.Godbless Lema, Mbunge wa Arusha alivunja Masharti ya kifungu cha 24 (c),(d) na (e) cha Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 pamoja na Kanuni ya 74(1) (a) na (b) ya kanun hiyo Kudharau Mamlaka ya Spika.

Kwa upande wa Mhe.John Heche alivunja kanuni ya 72 (1) na 68(10) ya kanuni za Bunge kwa kuendelea kusimama na kuomba mwongozo kwa jambo ambalo limekwishatolewa mwongozo na kuongeza kuwa vitendo hivyo vilivuruga shughuli za Bunge.

Kwa mujibu wa maelezo ya kamati hiyo Mhe.Halima Mdee, Mhe.Tundu Lissu,Mhe Pauline Gekul  na Mhe.Ester Bulaya walivunja masharti ya kifungu cha 24 (c), (d) na (e) cha sheria ya Haki,Kinga na Madaraka ya Bunge Sura ya 296 na Kanuni ya 72 (1)68 (10), 60(2) na 12 na 74(1) (a) na (b) kwa kusimama na kuendelea kuomba mwongozo kwa jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi, kuzungumza bila kufuata utaratibu na kudharau Mamlaka ya Spika.

Kufuatia uchunguzi huo Bunge kupitia kamati hiyo limeazimia kuwa Mhe. Ester Bulaya na Mhe.Tundu Lisu wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge la Kumi na Moja vilivyobaki kuanzia tarehe 30 Mei , 2016 pamoja na vikao vyote vya Mkutano wa Nne wa Bunge la Kumi na Moja kwa kuwa walipatikana na makosa ya ukiukwaji wa Kanuni na kuonyesha dharau kubwa kwa mamlaka ya Spika.

Aidha, Bunge limeazimia kuwa Mhe. Pauline Gekul, Mhe.Godbless Lema, Mhe.Zitto Kabwe na Mhe Halima Mdee wasihudhurie vikao vyote vya mkutano wa tatu wa Bunge kuanzia tarehe 30 Mei 2016.

Aidha  Bunge limeazimia Mhe.John Heche asihudhurie vikao kumi mfululizo vya Mkutano wa Tatu wa Bunge hilo kuanzia Mei, 30, 2016 kwa kuwa alipatikana na kosa moja na pia kwa kuwa alitoa ushirikiano kwa kamati kwa kufika na kujibu maswali yote kama alivyoulizwa pamoja na kuheshimu vikao vya kamati na Mwenyekiti aliyeongoza vikao hivyo.

Pamoja na adhabu hizo Kamati hiyo imetoa maoni na mapendekezo kuwa Bunge liandae mafunzo ya kutosha kwa wabunge wote kuhusu matumizi ya uzingatiaji sahihi wa kanuni sahihi wa kanuni za Kudumu za Bunge hasa kanuni za majadiliano ndani ya Bungeni.

Aidha, Kamati hiyo imesema kuwa ipo haja ya kutungwa kwa kanuni za maadili kwa wabunge wote kama kifungu cha 12 A Cha Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge kinavyoelekeza ili kuweza kudhibiti nidhamu kwa wabunge kwa kuhakikisha heshima na hadhi ya Bunge inadumishwa.

Kwa upande wao baadhi ya wabunge wakichangia kwa nyakati tofauti kuhusu suala hilo wamesema kuwa ipo haja ya Bunge kurudisha heshima yake kwa wabunge wote kuheshimiana na kutoa michango yenye staha kwa kuzingatia nafasi walizonazo katika jamii.

Wamesema kuwa michango wanayoitoa ndani ya Bunge hilo lazima ijikite katika masuala yanayowahusu wananchi wanaowawakilisha badala ya mambo yanayochochea vurugu na kulifanya Bunge lipoteze heshima yake katika jamii.

Aidha, wabunge hao wamekubali kwa kauli moja kuanza upya kuzingatia kanuni zinazoendesha vikao vya Bunge huku wakimtaka Spika wa Bunge au Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutosita kuchukua hatua za haraka kwa mbunge yeyote atakayekiuka utaratibu na kanuni zilizowekwa.

Serikali Yapiga Marufuku Pombe Ya Viroba ya Kwenye Mifuko Ya Plastiki


Mifuko ya plastiki inayofungasha pombe maarufu kama ‘viroba’ imepigwa marufuku na Serikali kuanzia mwakani. 

Sambamba na hilo Serikali pia, imepiga marufuku moja kwa moja utengenezaji, usambazaji, uingizaji nchini wa mifuko ya plastiki kuanzia mwaka huo.

Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba aliwaambia wanahabari jana sehemu kubwa ya mifuko hiyo inayotolewa bure imekuwa ikichangia uchafuzi wa mazingira kwa kiasi kikubwa.

Wakati Makamba akiyasema hayo, Februari mwaka huu Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Luhaga Mpina aliondoa zuio la matumizi ya mifuko ya plastiki akisema kuwa itaziweka rehani ajira za Watanzania wanaofanya kazi kwenye viwanda vinavyotengeneza mifuko hiyo.

Pia, Mpina alisema itapunguza kasi ya uwekezaji wa viwanda vilivyowekeza katika bidhaa hiyo.

Akizungumza katika siku ya Mazingira Afrika, Mkurugenzi wa Mazingira, Dk Julius Ningu alisema maamuzi hayo yamelenga kulinda viwanda vilivyoajiri mamia ya Watanzania, tofauti na nchi nyingine zinazotegemea wazalishaji wa nje ya nchi.

Makamba akizungumzia uamuzi mpya wa kuzuia mifuko ya plastiki, alisema matumizi ya mifuko inayofungashia vileo na inayotumika katika matumizi mengine husambaa na kuchafua mazingira. Alisema mifuko ya plastiki inatajwa kuziba mifereji na kusababisha mafuriko na athari nyingine za mazingira.

“Leo (Jana), tumeamua kutangaza ili kuwaanda wahusika wasiendelee kuwekeza katika mifuko hii badala yake wasubiri utaratibu mwingine utakaowekwa na Serikali,” alisema Makamba na kuongeza kuwa:

 “Asilimia kubwa ya uchafu kwenye nyanzo vya maji, mito, maziwa na fukwe za bahari ni mifuko ya plastiki.” 

Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli, alisema Serikali inakamilisha majadiliano ya ndani na baadaye itawahusisha wadau kuhusu dhamira ya kupiga marufuku ya moja kwa moja mifuko hiyo.

Alifafanua kwamba Serikali itatoa muda kwa walioajiriwa, kujiajiri na kuwekeza kwenye biashara ya mifuko hiyo ili kujiandaa kuacha shughuli hizo na badala yake itawezesha mazingira ya utengenezaji na upatikanaji wa vifungashio mbadala.

“Kwa wanaotengeza mifuko hii na kuiuza katika soko la nje hatuna tatizo nao waendelee. Ila kwa soko la ndani hawataruhusiwa kufanya hivyo.Zuio hili litakuwa la kisheria siyo kwa maneno,” alisisitiza Makamba. 

Aliongeza kuwa katika kuonyesha Serikali imedhamiria kupambana na hali hiyo wizara yake imeamua kutuma timu ya watu watano kwenda Rwanda kujifunza namna bora ya kudhibiti matumizi na kuzuia mifuko hiyo tangu mwaka 2008.

Waziri huyo alitoa wito kwa watengenezaji, wasambazaji na waagizaji wa mifuko hiyo kujiandaa na zuio hilo na katika siku zijazo Serikali itatoa utaratibu na maelekezo ya tarehe ya kuanza zuio huku taratibu nyingine za kina zikifuata ili kuondoa mkanganyiko.

 Katika hatua nyingine, Makamba alisema maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika Juni 5 kila mwaka hayatafanyika kitaifa badala yake wizara imewaelekeza wakuu wa mikoa kufanya maadhimisho katika maeneo yao.

 “Tumewapa miongozo kuhusu utekezezaji wa shughuli hizo za maadhimisho zinazolenga kutoa hamasa ya hifadhi ya mazingira hususan nyanzo ya maji amabayo ni muhimu kwa viumbe hai,” alisema Makamba.

Kwa mujibu wa Makamba, kauli mbiu ya mwaka huu kitaifa juu ya maadhimisho hayo ni ‘ tuhifadhi vyanzo vya maji kwa uhai wa taifa letu’aliwashauri na kuwataka Watanzania kutumia siku hiyo kupanda miti, kudhibiti uchomaji wa misitu 

Ofisa Mwandamizi Mazingira wa Nemc, Arnold Kisagala alisema nusu ya mifuko ya plastiki nchini inazalishwa na kuingizwa kutoka nchi jirani ya Kenya.

Alisema agizo la Waziri Makamba litawezekana, lakini linahitaji ushirikiano kutoka kwenye sekta zingine kwa kuwa viwanda vingi vya mifuko ya plastiki vipo Kenya.

"NEMC tayari tulishaanza mazungumzo na wazalishaji kuhusu mifuko ya plastiki,”alisema. 

Saturday, 28 May 2016

Wimbo wa 'Panya' Wakiponza Kitua cha EATV, Chapigwa Faini ya Milioni 3 na TCRA


Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), imevitoza faini vituo vya East Africa Television na Entertaiment FM (E- FM) baada ya kukiuka kanuni za utangazaji.

Akisoma nakala ya hukumu hiyo mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda alisema baada ya kupitia maelezo ya utetezi kutoka kwa viongozi wa vituo hivyo, kamati hiyo imeamua kuitoza EATV faini ya Sh3 milioni na Sh4 milioni kwa E-Fm.

“Pamoja na adhabu hiyo tumetoa onyo kali kwa kukiuka kanuni ya maudhui, lakini pia endapo kosa hili litajirudia tunaahidi kutoa adhabu kali zaidi,” alisema.

Katika maelezo ya awali ya hukumu hiyo, Mapunda alisema adhabu ya EATV imetolewa baada ya kituo hicho kupitia kipindi chake cha muziki mnene kurusha video ya wimbo wa Panya wa kundi la muziki la Bracket kutoka nchini Nigeria uliomshirikisha msanii Techno.

“Baadhi ya mavazi yaliyotumika katika wimbo huo hayaendani na maadili ya Kitanzania. Na kwa upande wa E-FM wameadhibiwa baada ya kurusha kipindi cha Ubaoni kilichotoa simulizi ya msichana mchawi aliyekiri kuua,”alisema Mapunda.

Baada ya kupokea nakala ya hukumu hiyo, Mkurugenzi wa EATV, Regina Mengi alisema hawana tatizo na adhabu hiyo na kwamba, atalifikisha suala hilo kwa uongozi wa kampuni yao.

“Bado siwezi kujibu lolote, uamuzi wa kuikubali au kukata rufaa itategemea na uamuzi wa bodi,” alisema.

Mkurugenzi wa E-FM, Scolastica Mazula alisema ameridhishwa na hukumu iliyotolewa, hivyo haoni kama kuna sababu ya kukata rufaa.

Mamlaka hiyo imevitaka vyombo vyote vya utangazaji nchini kuzingatia maadili na taratibu za sheria zinapofanya kazi ili kuepuka kuleta athari katika jamii.

Watumishi Wavaa Vimini, vipedo, t-shirt, Jeans Kufyekwa Mshahara

HALMASHAURI ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, imepiga marufuku watumishi wote wa halmashauri hiyo kuvaa mavazi ambayo hayana maadili katika sehemu za kazi na kwamba atakayebainika atarudishwa nyumbani na kukatwa mshahara wa siku husika.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Adriano Jungu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Bomani wilayani Muheza juzi.
  
Alisema lazima mtumishi ahakikishe staha ya mavazi aliyovaa kabla hajaingia kazini katika ofisi yake na kwamba mtumishi atakayekiuka kuvaa mavazi ambayo hayaendani na maadili sehemu ya kazi atachukuliwa hatua za kinidhamu.
  
Akieleza zaidi, Jungu alisema kuwa mavazi ambayo hayaruhusiwi kwa watumishi ndani ya halmashauri yake ni pamoja na fulana, suruali za jeans, vimini, vitop, Pedo, yeboyebo, kaptula (pensi) na kandambili kwa sababu kuvaa vyote hivyo ni kinyume cha maadili ya utumishi.
  
Alisema kuwa mtumishi yeyote katika Halmashauri ya Wilaya ya Muheza kabla ya kuingia kazini lazima aangalie mavazi aliyovaa na kwamba sheria iko katika waraka wa utumishi wa umma namba 3 wa mwaka 2007 na lazima watumishi waheshimu waraka huo.
  
Jungu alisema mtumishi yeyote katika halmashauri ya Wilaya ya Muheza ambaye atakiuka sheria hiyo kwa kuvaa nguo za kihuni wakati wa kuingia kazini basi atarudishwa nyumbani na atakatwa mshahara wake wa siku hiyo.
  
Alisema kuwa lazima watumishi waheshimu sehemu ya kazi kwa kuvaa nguo za heshima ikiwamo wanawake na wanaume kwa kuwa ofisi hizo wanaingia watu wenye heshima ikiwamo wazee sasa haiwezekani mtumishi mwanamke anaingia ofisini na kimini kinachofika katika magoti na hivyo mapaja yake yanaonekana sasa anamtamanisha nani.
  
Jungu alisema kuwa kwa wanaume nao lazima wawe na nidhamu ya kuvaa mavazi ya heshima na siyo kuvaa mavazi ya jeanz mlegezo na flana zinazowabana ni marufuku kabisa katika halmashauri ya Muheza.
  
Alisema ataanza kupita kila ofisi Jumatatu Mei 30 asubuhi kwa ajili ya kuwakagua mavazi yao watumishi hao wakiwamo wanawake na wanaume ili kukomesha tabia kama hiyo ambayo ni kinyume na maadili ya utumishi wa umma hapa Tanzania.
  
Jungu alitoa onyo kwa kupiga marufuku watumishi kufika kazini wakiwa wamelewa na mtumishi akibanika amefanya hivyo na ushaidi upo atampeleka hospitali kupimwa na akibainika atamtumbua jipu hadharani kwani serikali ya awamu ya tano ni ya  hapa kazi tu.

Mazito Yaibuka Mauaji ya Dada yake Bilionea Msuya .........Yadaiwa Binti wa Kazi Alitoweka Mchana, Usiku Dada Akachinjwa

Siku moja baada ya kifo cha dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth imebainika kuwa msaidizi wa ndani aliondoka saa sita mchana kwa kuacha funguo nyumba ya jirani.

Akizungumza nyumbani kwa dada wa marehemu, Mbezi Juu, mama mdogo wa marehemu Lilian Benjamin alisema msaidizi huyo alimpigia simu bosi wake mchana na kumwambia anaondoka na hataendelea na kazi.

Alisema marehemu alilazimika kuomba ruhusa mapema kazini ili arudi nyumbani kwake Kibada lakini ilimlazimu kukaa nje ya nyumba kwa saa mbili baada ya kufika saa tisa alasiri na kukuta mlango umefungwa.

Mama huyo alisema baada ya kusubiri kwa muda aliwauliza majirani wakamweleza kuwa walipelekewa funguo na mwanafunzi wasiyemfahamu akadai kuwa alipewa na dada mmoja aliyemuelekeza aipeleke nyumba hiyo.

Haifahamiki mpaka sasa mahali alipo mfanyakazi huyo anayedaiwa kuwa mwenyeji wa Arusha.

Dada mkubwa wa marehemu, Happy Msuya alisema marehemu aliwaeleza mambo hayo baada ya kupigiwa simu na msichana huyo wa kazi.

Dada mwingine wa marehemu ambaye ni wa nne kuzaliwa kati ya watoto saba wa Elisaria Msuya, Ester, alisema wauaji hao hawakuwa na nia ya kuiba, bali ni kuua kwa sababu hawakuchukua kitu chochote zaidi ya televisheni ambayo nayo waliitupa mbali na nyumbani.

Ester alisema mara ya mwisho kuonana na marehemu ilikuwa Mei saba walipokutana benki na mazungumzo yao yalihusu hali ngumu ya maisha. Alisema hakuwahi kumwambia kama ana ugomvi na mtu kwa sababu alikuwa mpole na msiri.

Akielezea tukio hilo alisema inaonekana kulikuwa na purukushani kubwa chumbani kwa sababu besela la kitanda lilikuwa limevunjika na neti ilikuwa imetoka, huku nyaraka zikiwa zimepekuliwa na kusambazwa karibu kila kona ya chumba.

“Walikuja kuua, kuna kitu walikuwa wanatafuta katika nyaraka pia, ooh... Aneth umekufa kinyama, umechinjwa kama mnyama,” Ester alishindwa kuendelea na kuanza kulia na baadaye kidogo alisema wauaji walimkata marehemu koromeo lakini hawakutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Simulizi ya mtoto 
Mtoto wa marehemu mwenye umri wa miaka minne ambaye alikuwa akiishi na mama yake alisema: “Walikuja watu watano weusi usoni, wakanifanya na kitu shii usoni, nikalala kwenye kiti mbu wameniuma hadi niliposikia gari la shule likiita pipii, nikaamka na nikamuamsha mama anivalishe nguo za shule lakini akakataa kuamka, ”alisema mtoto huyo na kuongeza.

“Nikavaa mwenyewe nguo za shule na nikamwambia mama nitaendaje shule huku sijafanya “Home work” lakini mama hakujibu, mbu walining’ata pale kwenye kochi nilipolala, nikatoka nje nikakuta gari limeshaondoka, nikaenda kwa mama Salum,”alisema.

Alisema alienda huko akale kwa sababu njaa ilikuwa inamuuma hakula jana yake baada ya ‘wageni’ hao kuja na yeye kulala.

Alieleza kuwa alipowaambia mama yake hamjibu amelala tu alirudi na dada ambaye amemsahau jina kutoka hapo kwa mama Salum ambaye alipofika nyumbani kwao na alipomuona mama yake alianza kupiga kelele.

Ester alisema mwili wa marehemu utasafirishwa Jumatatu ijayo kuelekea kijijini kwao Kairo, Simanjiro mkoani Manyara.

Mtu wa karibu na familia ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema mbali ya kaka yao Erasto kuuawa kwa risasi, dada yao Ester akiwa na mumewe katika Baa ya Hongera, Dar es Salaam alipigwa risasi na kunusurika kufa.

Thursday, 26 May 2016

Silaa adai wafuasi wa Chadema walitishia kuchoma nyumba


ALIYEKUWA mgombea ubunge wa Ukonga, Jerry Silaa (CCM) amedai kuwa wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) walimtishia kuchoma moto nyumba yake wakati wa Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka jana.

Silaa alieleza hayo jana katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, wakati akitoa ushahidi wa kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa jimbo hilo, Mwita Waitara (Chadema).

Alitoa ushahidi huo kwa njia ya kiapo baada ya Jaji Fatuma Msengi kutupilia mbali pingamizi la upande wa walalamikiwa waliokuwa wanapinga kupokewa kwa kiapo hicho kwa kuwa kina mapungufu kisheria.

Katika kiapo hicho, Silaa anaeleza kuwa, Oktoba 27 mwaka jana katika kituo cha kujumlishia kura cha Pugu Sekondari, kulikuwa na idadi kubwa ya wapiga kura wa Chadema wakiwa wamesimama mita 20 kutokea usawa wa kituo hicho.

Alidai kuwa wafuasi hao walianza kuwatishia Mawakala na Msimamizi wa Kituo, jambo lililosababisha Polisi washindwe kufanya kitu zaidi ya kuwaonya, ndipo mjibu maombi wa pili na wenzake wakasema hawatopokea matokeo na watachoma moto nyumba yake pamoja na kituo hicho.

Silaa ambaye aliwahi kuwa, Meya wa Manispaa ya Ilala, alidai hadi Oktoba 27, baadhi ya vituo vilikuwa havijakusanya matokeo jambo lililosababisha aandike barua kwenda kwa Msimamizi wa Kituo kuomba mchakato wa kuhesabu kura urudiwe.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Asema Hakuna UGAIDI Jijini Humo.......Adai Mauji Msikitini ni Tukio ya Uhalifu wa Kawaida Kama Yalivyo Mengine


Wakati Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza likiwashikilia watu 14 kwa tuhuma za mauaji ya watu watatu katika Msikiti wa Rahman uliopo Ibanda, Kata ya Mkolani mjini Mwanza, Mkuu wa mkoa huo, John Mongella amesema mauaji hayo hayana sura ya ugaidi.

Mongella amesema mauaji hayo hayafanani na vitendo vya aina hiyo, hivyo ni vigumu kuyahusisha na ugaidi bali ni uhalifu kama ulivyo mwingine.

Bila kufafanua, alisema mauaji mengine yanasababishwa na ndugu na jamaa za marehemu. Kadhalika, aliwataka viongozi wa mtaa huo kuimarisha vikundi vya ulinzi shirikishi vitakavyoweza kukabiliana na uhalifu wa aina hiyo.

Mauaji hayo yalitokea Mei 18, saa mbili usiku wakati waumini hao wakiwa msikitini wanaswali.

Waliouawa katika tukio hilo ni Imamu wa msikiti huo, Feruz Ismail, Mbwana Rajabu na Khamis Mponda, wakazi wa Ibanda na kumjeruhi Ismail Ghati.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema watuhumiwa hao walikamatwa katika msako dhid ya wahalifu unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo.

Hata hivyo, alisema bado hawajamkamata mtuhumiwa aliyempiga risasi Mwenyekiti wa Mtaa wa Bulale, Kata ya Buhongwa jirani na ya Mkolani. 

Mwenyekiti huyo Alphonce Nyinzi (48), alipigwa risasi Mei 22, saa moja usiku muda mfupi baada ya kumaliza kuongoza kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mtaa huo.

Kamanda Msangi aliwataka wananchi kutoa ushirikiano ili kuwabaini watu wanaoendeleza uhalifu katika mkoa huo.

“Nawaomba wananchi watupatie ushirikiano maana sisi wenyewe hatuwezi kufanya kazi bila ya kupata ushirikiano wao kwa sababu jamii yenyewe ndiyo inayoishi na watu hao, tuleteeni taarifa za uhalifu tutazifanyia kazi,” alisema.

Kwa kipindi cha wiki mbili mkoani Mwanza, watu 12 wameuawa kwa kukatwa mapanga na shoka, mmoja kwa kupigwa risasi na watu wasiofahamika.

Ester Bulaya Achafua Hali ya Hewa Bungeni Baada ya Kumfananisha Waziri Maghembe na TISHU


Mbunge wa Bunda Mjini (Chadema), Ester Bulaya jana alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kusema kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe ni mzigo na mwepesi kama ‘tishu’ kwa sababu hana uwezo wa kusimamia mambo mazito yaliyopo katika wizara hiyo, kama vile migogoro ya wananchi na hifadhi za Taifa.

“Huyu waziri ni mzigo kama alivyowahi kusema (Abdulrahman) Kinana. Mimi nasema yeye ni mwepesi kama tishu, hawezi kuisaidia wizara hii nyeti,” alisema mbunge huyo jana wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama alisimama na kuomba mwongozo wa mwenyekiti juu ya mbunge huyo kutumia maneno ya kuudhi ambao uliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliyemtaka Bulaya kufuta neno mwepesi kisha aendelee na hotuba yake. Hata hivyo, Bulaya alikataa kufuta neno hilo na kusema wabunge hawaamuliwi maneno ya kutumia.

Chenge aliendelea kumsihi mbunge huyo kufuta neno hilo na katika mabishano hayo yaliyodumu kwa dakika tatu, baadaye, Bulaya alikubali kuondoa neno ‘tishu’ na kuliacha neno mwepesi na kuruhusiwa kuendelea kuchangia.

“Mwenyekiti sitafuta neno mwepesi, kama neno ‘tishu’ linawakera basi naliondoa libaki mwepesi,” alisema Bulaya.

Katika mchango wake, Bulaya alisema wananchi wanaoishi katika hifadhi zilizopo jimboni mwake wananyanyaswa na askari wanyamapori wakati Serikali imeshindwa kuwatengenezea mazingira mazuri ya kuishi.

Alimtaka waziri huyo kushughulikia kero zote zinazowakabili wananchi wa Bunda akisema Serikali haiendeshwi kwa maneno matupu, bali vitendo na dhamira ya dhati ya kuwahudumia wananchi.

“Tatua matatizo jimboni kwangu ili niweze kukupima kama wewe ni mzito au mwepesi,” alisema mbunge huyo akimwambia Profesa Maghembe.

Baada ya Bulaya kumaliza muda wake, mbunge aliyefuatia alikuwa Abdallah Ulega wa Mkuranga (CCM) ambaye alisema kuna haja ya wabunge kupimwa kama wamelewa getini ili kujua akili zao.

“Kijana aliyefunzwa vizuri hawezi kumtukana mzee kama yule (Maghembe). Kama suala ni uwaziri basi aangalie hata umri wake kabla ya kuzungumza... Naungana na aliyesema wabunge tupimwe vilevi kabla hatujaingia humu ndani. Unaweza kujenga hoja yako bila kutukana, huhitaji kutukana ili waziri atekeleze madai yako,”alisema mbunge huyo.

Saturday, 21 May 2016

Sukari "Yakauka" Manispaa Ya Kigoma-ujiji, Hata Ile Ya Kilo Sh. Elfu 5,000 Hakuna

Mkoa wa Kigoma umekaukiwa na sukari kuanzania Ijumaa Mei 20, 2016 na taarifa ya Ofisi ya Biashara ya Mkoa, imesema, Wakazi wa Manispaa ya Kigoma –Ujiji wavumilie hadi mwisho wa mwezi huu wa Mei.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, kabla ya siku ya Ijumaa, sukari iliuzwa kwa bei ya shilingi elfu 5,000 kwa kilo, kwenye eneo la Manispaa ya Kigoma-Ujiji, lakini Ijumaa maeneo yote ya manispaa hiyo hayakuwa na sukari hata hiyo ya shilingi elfu 5.

Akizungumzia uhaba huo mkubwa wa sukari mkoani humo, Afisa biashara wa mkoa wa Kigoma Deogratius Sanga, amekiri kuwepo kwa uhaba huo na kuwataka wananchi wa Manispaa hiyo kwua wavumilivu wakati serikali ya mkoa inatafutia ufumbuzi tatizo hilo. 

“Taarifa toka bodi ya sukari ni kwamba ile sukari iliyoahidiwa na waziri mkuu itafika mwisho wa mwezi huu, na tunategemea kuanzia mwezi ujao tatizo hili litakwisha”.alisema Sanga.

Majina Ya Kidato Cha Sita 2016 Wanaotakiwa Kujiunga Na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria......Tarehe ya Kuripoti Kambini ni Tarehe 1 Hadi 5 Juni


Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2016, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria.

Sanjari na uchaguzi huo, JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo kwa muda wa miezi mitatu na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 - 05 Juni 2016.

Vijana waliochaguliwa, wamepangiwa katika Kambi za JKT Rwamkoma – Mara, JKT Msange – Tabora, JKT Ruvu – Pwani, JKT Makutupora – Dodoma, JKT Mafinga – Iringa, JKT Mlale – Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba – Tanga, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila – Kigoma.

Aidha, wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) wanatakiwa kuripoti Kambi ya JKT RUVU, iliyopo Mlandizi mkoani Pwani, ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

JKT linawataka vijana hao kuripoti makambini wakiwa na nguo za michezo kama vile ‘track suit’, bukta, raba pamoja na nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa kwenye makambi yenye baridi kama JKT Makutupora, JKT Mafinga, JKT Mlale, JKT Kanembwa na JKT Mtabila.

Mkuu wa JKT anawakaribisha vijana wote waliochanguliwa ili waweze kujiunga na vijana wenzao katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, uhodari, stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa letu.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Habari na Uhusiano

Makao Makuu ya JKT

Tarehe 20 Mei 2016

Friday, 20 May 2016

Breaking News: Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Waziri Wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga Baada Ya Kuingia Bungeni Akiwa Amelewa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Dar es salaam

20 Mei, 2016

Kigogo wa CCM Ataka Maalim Seif Sharif Hamad Akamatwe

Kigogo wa CCM aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Sukwa Said Sukwa amevishauri vyombo vya dola visiwani Zanzibar kumchukuliwa hatua haraka Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kwa kauli yake aliyoihusisha na kosa la uhaini.

Sukwa aliitaja kauli ya Maalim Seif aliyoitoa alipokuwa akihutubia katika mkutano wa hadhara kisiwani Pemba kuwa Dk. Ali Mohamed Shein hatamaliza kipindi chake cha urais mwaka 2020 na kwamba ni dikteta.

Sukwa amesema kuwa kauli hiyo ya Maalim Seif haipaswi kupuuzwa hata kidogo kwakuwa kauli kama hizo ni zaidi ya sumu.

“Sivilazimishi vyombo vya dola kufanya ninavyotaka, lakini tunashauri tu visipuuze ushauri wetu kwa sababu ulimi wa mtu unaweza kuwa sumu hatari kuliko matendo yake,” Sukwa aliliambia gazeti la Raia Tanzania.

Maalim Seif amekuwa akifanya mikutano kuwataka wananchi kumuunga mkono kuikataa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Shein, akieleza kuwa uchaguzi wa marudio haukuwa wa hak

Diamond Atajwa Kuwania Tuzo za BET 2016

Diamond Platinumz anaendelea kupaa katika ulimwengu wa muziki kimataifa ambapo mwaka huu pia nyota yake imeng’aa kwenye tuzo kubwa za Black Entertainment Television (BET 2016).

 

Mwimbaji huyo ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa akichuana na wasanii wengine nguli Afrika ambao ni pamoja na AKA kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest wa Afrika Kusini Black Cofee wa Afrika Kusini, Yemi Alade wa Nigeria, Wizkid wa Nigeria, Mzvee wa Ghana na Serge Beynaud wa Ivory Coast.

Tuzo hizo zitafanyika Juni mwaka huu nchini Marekani ambapo Diamond pia ametajwa kati ya watakaotumbuiza.

Diamond Atajwa Kuwania Tuzo za BET 2016

Diamond Platinumz anaendelea kupaa katika ulimwengu wa muziki kimataifa ambapo mwaka huu pia nyota yake imeng’aa kwenye tuzo kubwa za Black Entertainment Television (BET 2016).

 

Mwimbaji huyo ametajwa kuwania kipengele cha Best International Act: Africa akichuana na wasanii wengine nguli Afrika ambao ni pamoja na AKA kutoka Afrika Kusini, Cassper Nyovest wa Afrika Kusini Black Cofee wa Afrika Kusini, Yemi Alade wa Nigeria, Wizkid wa Nigeria, Mzvee wa Ghana na Serge Beynaud wa Ivory Coast.

Tuzo hizo zitafanyika Juni mwaka huu nchini Marekani ambapo Diamond pia ametajwa kati ya watakaotumbuiza.

Thursday, 19 May 2016

Wanaharakati na Wanasiasa Waaswa kuacha kubeza Mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano Chini ya Rais Magufuli


Wanaharakati na wanasiasa wanaobeza juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano, wametakiwa kuacha kuupotosha umma juu ya mafanikio yaliyofikiwa na Serikali hiyo chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam leo na Afisa Habari wa CZI- information And Media Consults Co. Ltd, Augustino Matefu  wakati wa mkutano na vyombo vya Habari uliolenga kueleza mafanikio ya Serikali ya awamu ya tano.

Alisema Serikali ya awamu ya tano imeonesha mafanikio makubwa katika sekta ya ukusanyaji mapato, elimu, miundombinu, afya na kujenga uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma.

Hivyo alitoa wito kwa Watanzania wote kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano na kuwapuuza wanaharakati na wanasiasa hao wanaunga mkono wale wasioitakia mema Tanzania na Serikali ya awamu ya tano kwa ujumla.

Alisema katika sekta ya mapato, Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miezi saba iliyopita imefanikiwa kuongeza mapato kutoka shilingi bilioni 900 kwa mwezi kabla ya utawala wake hadi shilingi trilioni 1.5 kwa sasa.

 “Rais wa awamu ya tano ameondoa michango yote ya shule za msingi na Sekondari ambayo ilikuwa kero kwa wazazi na wananchi kwa ujumla”alisisitiza Matefu

Katika mpango wa elimu bure Matefu alibainisha kuwa umesaidia kuongeza idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kujiunga na elimu ya msingi na ile ya Sekondari.

Aliongeza kuwa Rais Magufuli amejenga Barabara ya Mwenge hadi Moroko kwa Fedha za ndani hali inayoonyesha kuwa Serikali inayo dhamira ya dhati ya kuwaletea maendeleo  wananchi wake.

Alisema hata Hosipitali ya Taifa Muhimbili imepatiwa  vitanda vya kutosha na hivyo kuondoa tatizo la msongamano katika wodi ya wazazi na kwa sasa wagonjwa wanalala kwenye vitanda.

“Mambo mengine yaliyofanywa na Serikali katika kipindi hiki yanalenga kuinua maisha ya wananchi wa chini ikiwemo kujenga mazingira mazuri yatakayowezesha shughuli za uzalishaji kuongezeka ili kuinua hali ya maisha ya wananchi”alisema Matefu.

Kujengwa kwa utamaduni wa uwajibikaji miongoni mwa watumishi wa umma ni moja ya mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya tano ambapo sekta ya utumishi wa umma imeonesha mabadiliko makubwa katika uwajibikaji.

Watu Watatu Wauawa Kwa Kukatwa Mapanga na Mashoka Jijini Mwanza


Mnamo tarehe 18.05.2016 majira ya saa 20:30hrs katika msikiti wa masjid rahman uliopo ibanda relini mtaa wa utemini @ mapankini kata ya mkolani wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza. 

Watu wasiozidi 15 wakiwa wamevalia mavazi ya kuficha uso wakiwa na mapanga, shoka na bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia ghafla katika msikiti tajwa hapo juu wakati waumini wa msikiti huo wakiwa wanaswali na kuzima taa na kutoa sauti wakisema “kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi ?” na hapo hapo wakaanza kuwakata kwa mapanga baadhi ya waumini katika sehemu mbalimbali za miili yao. 

Walipata majeraha makubwa kichwani, shingoni na mikononi na walipoteza maisha yao papo hapo na mmoja kupata majeraha sehemu za kichwani na kukimbizwa hospitali ya wilaya ya nyamagana (butimba). 

 

Waliouawa, 1. Feruz ismail elias  mika 27, muha imamu wa msikiti huo na mkazi wa ibanda relini, 2. Mbwana rajab miaka 40, mbondei mfanyabiashara na mkazi wa ibanda, 3. Khamisi mponda miaka 28 dereva wa kiwanda cha samaki (TFP), mkazi wa mkolani, wote walijeruhiwa sehemu za kichwani, shingoni na mikononi. 

Aliyejeruhiwa ni ismail abeid @ ghati miaka 13, mkurya mwanafunzi wa madrasa katika  shule ya kiislamu itwayo jabar hila iliyoko maeneo ya Nyasaka aliyepata majeraha kichwani na anapata matibabu hospitali ya Nyamagana.

 

Kutokana na hali hiyo, waumini wengine walifanikiwa kukimbia huku wakipiga mayowe yaliyopelekea wahalifu hao kukimbia na kurusha ndani ya msikiti chupa mbili za konyagi zilizokuwa na petroli na tambi za moto, chupa moja ililipuka lakini haikuleta madhara makubwa.

 

Jeshila la polisi  limewakamata washukiwa watatu kwa ajili ya kuwahoji kuhusiana na tukio hilo, huku msako mkali wa kuwasaka watu wengine walio husika kwa namna moja au nyingine kwenye mauaji hayo ukiwa bado unaendelea. 

Napenda kuwaeleza  wananchi watulie wakati tukiendelea na upelelezi wa tukio hili, na natoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu wa mauaji hayo ili tuweze kuwakamata. 

Pia nashauri na kusisitiza kuwepo na kamati za ulinzi na usalama katika nyumba za ibada, kumbi za starehe pamoja na mitaa yao. Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo.

Imesainiwa na:

……………………….

Sacp: Ahmed Msangi

Kamanda wa Polisi (m) Mwanza.

Wednesday, 18 May 2016

Zitto Kabwe, Halima Mdee na John Heche Wawekwa Kitimoto.....Wahojiwa Kwa Dadkia 90 Kwa Kufanya Fujo Bungeni

MBUNGE wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto (ACT-Wazalendo) na wenzake wawili, jana wamehojiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika kwa kufanya fujo bungeni kuhusu suala la Bunge kutorushwa ‘live’.

Mbali na Zitto, wengine waliohojiwa ni pamoja na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) na Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema). Wabunge hao walihojiwa kwa tuhuma za kufanya fujo bungeni wakati ilipotolewa hoja ya Bunge kutorushwa moja kwa moja ‘live’, akiwa pamoja na wabunge wawili; Mdee na Heche.

Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya kamati hiyo, kimesema Zitto alihojiwa na kamati hiyo kwa muda wa zaidi ya saa moja kwa makosa mbalimbali, ikiwamo kufanya fujo bungeni Januari 27, mwaka huu.

Taarifa hizo zilieleza kuwa Zitto alifanya fujo hizo baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge, kuahirisha kujadili hoja ya serikali iliyowasilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, kuhusu Bunge kutorushwa ‘live’.

Hatua hiyo inatokana na hoja iliyowasilishwa na Zitto aliyetaka kuahirishwa kujadili hotuba ya Rais kutokana na kauli ya Waziri Nape ya kutorushwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge.

Zitto, alihojiwa na kamati hiyo ya Mkuchika kwa kilichoelezwa alisimama na kuomba mwongozo kuhusu jambo ambalo limekwishatolewa uamuzi kinyume na Kanuni ya 72 (1) na 68 (10 ya Kanuni za Kudumu za Bunge toleo la Januari 2016.

Mbali na hilo pia anadaiwa kusimama na kuzungumza bila utaratibu kinyume na Kanuni ya 60 (2) na 12 ya Kanuni za Kudumu za Bunge, jambo ambalo lilileta fujo na kuvunja shughuli za Bunge.

Katika barua za mwito zilizosainiwa na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, Mei 12, mwaka huu, inaelezwa kwamba pamoja na mambo mengine na Mwenyekiti wa Bunge kumsihi mbunge huyo bado aliendelea kuzungumza na kusimama ikiwa ni kuonesha dharau kwa mamlaka ya Spika na shughuli za Bunge kinyume na kifungu namba 24 (d) na (e) cha Sheria ya Kinga na Haki za Bunge.

Barua hiyo ilieleza kuwa kutokana na vitendo hivyo vinavyokiuka Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, Sura namba 296 na Kanuni za Bunge, wabunge hao walionywa kuwa endapo wasingefika mbele ya kamati hiyo jana hatua za kisheria zingechukuliwa dhidi yao kwa mujibu wa kifungu cha 15 na 31 (1)(a) na sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge.

Sakata la Lugumi: CHADEMA Yajipanga Kumng'oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema uzito wa Rais John Magufuli kumwajibisha Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga kutokana na kutajwa kuhusika na Kampuni ya Lugumi inayodaiwa kulitapeli Jeshi la Polisi, utasababisha waanze harakati za kumng’oa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu aliwaambiawaandishi wa habari jana kuwa Rais John Magufuli hana budi kuchukua hatua haraka kumwajibisha Waziri Kitwanga kama alivyofanya kwa watumishi wengine wa umma katika operesheni ya kutumbua majipu.

Waziri Kitwanga anadaiwa kuwa na hisa kwenye Kampuni ya Infosys Ips Tanzania Limited ambayo ilipewa zabuni ya kutoa huduma za kitaalamu na Kampuni ya Kimarekani ya Biometrica kuhusu uwekaji wa mashine za kielektroniki za kuchukua alama za vidole kwenye vituo 108 vya polisi. 

Mkataba wa kuweka mashine hizo uliingiwa kati ya Jeshi la Polisi na Kampuni ya Lugumi Enterprises ambayo ililipwa Sh34 bilioni kati ya Sh37 bilioni za mkataba, wakati kazi ya kufunga mashine hizo ilifanyika kwenye vituo 14 tu hadi wakati Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alipofanya ukaguzi.

Hata hivyo, kampuni hiyo inadai kuwa Kitwanga, ambaye ni mmoja wa waasisi wa Infosys, alijiondoa kwenye uendeshaji tangu mwaka 2010, wakati mkataba huo ulisainiwa mwaka 2011.

Chadema bado inaona kuwa Rais Magufuli anatakiwa kumwajibisha waziri huyo wa Mambo ya Ndani.

“Kama Rais akishindwa kuchukua hatua katika hili, Serikali itang’oka madarakani. Sisi Chadema tutaiondoa. Haiwezekani wakati Lugumi inachunguzwa mhusika mkuu (Kitwanga) aendelee kuwa waziri, tena wa wizara inayohusika na mkataba wa Lugumi,” alisema Mwalimu.

Mwalimu alisema, Rais anapaswa kujitokeza hadharani na kueleza uhusiano wake na Kitwanga na awaeleze Watanzania kuwa kutokana na uswahiba wao ndiyo sababu ya kutomchukulia hatua.

“Mbona anawatumbua marafiki wa wenzake? Kwa nini marafiki zake anashindwa kuwatumbua? Ukiwa kiongozi mwenye kubagua katika uamuzi ni hatari kwa uchumi wa Taifa, ni sawa na baba anayewabagua watoto wake matokeo yake ni kuzalisha chuki tu.”

Licha ya Mwalimu kutotaka kuweka wazi mpango huo, kwa mujibu wa Ibara ya 53 A(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, Bunge linaweza kupitisha azimio la kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu endapo itatolewa hoja kupendekeza hivyo.

 Kwa mujibu wa Ibara hiyo, hoja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu inapaswa kuungwa mkono na wabunge wasiopungua asilimia 20 ya wabunge wote.

Wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni 372, kati yao wabunge wa upinzani ni 118.

“Hilo tutalifanya iwapo tu Rais atashindwa kumwajibisha Kitwanga. Ila huyu waziri naye anapaswa ajipime mwenyewe ili kumlinda bosi wake (Waziri Mkuu). Afanye kama Edward (Lowassa-waziri mkuu mstaafu) aliamua kujiuzulu wadhifa wake ili kumlinda Jakaya (Kikwete-Rais wa Awamu ya Nne) kwa kosa ambalo yeye hakulifanya,” alidai Mwalimu.

Mwalimu alidai kwamba Serikali imezuia matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kuhofia uchafu wa viongozi, likiwamo sakata la Lugumi.

“Ndiyo maana tunasema CCM ni ileile maana wametumbua majipu, sasa imebaki mitoki. Ni kama imewashinda maana ipo sehemu mbaya,” alisema.

Licha ya mkakati huo wa Chadema, Aprili 19 mwaka huu, Kitwanga alisema kuwahahusiki katika sakata hilo na juzi alijibu hoja ya Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) lililomtaka ajiuzulu, akisema hawezi kuwajibu watoto ili kuonyesha tofauti yake na wao.

Katika maelezo yake, Mwalimu aliorodhesha utumbuaji ambao Rais Magufuli ameufanya tangu aingie madarakani, ukiwamo wa watendaji waliofanya vurugu tu katika vikao kwa kusisitiza kuwa ni ajabu kuona mpaka sasa hajamchukulia hatua yoyote Kitwanga wakati ukweli uko wazi kuwa anahusika na sakata la Lugumi. 

Baada ya ripoti ya CAG kuibua udhaifu huo kwenye mkataba, Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge iliunda kamati ndogo kufuatilia tuhuma hizo baada ya kutoridhishwa na maelezo ya Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi kuhusu mkataba huo.

Kampuni ya Infosys ni wakala wa kampuni maarufu duniani ya kutengeneza kompyuta ya Dell, ikijihusisha na usambazaji wa vifaa hivyo, matengeneza na utoaji huduma za kitaalamu.

Kaimu katibu mkuu huyo wa Chadema alisema, chama hicho pia kinajipanga kuanza ziara yake nchi nzima na ajenda kuu itakuwa kuanika mambo yote mabaya yanayofanywa na Serikali.

Polisi Akamatwa na Noti Bandia Zenye Thamani ya Sh. 870,000


ASKARI Polisi Ezekiel Dinoso (32) mkazi wa tarafa ya Mgeta, wilayani Mvomero mkoani Morogoro amekutwa na noti bandia za Sh 10,000 zenye thamani ya Sh 870,000, akijiandaa kuzitumbukiza katika akaunti ya mtandao wa Tigo Pesa katika duka mojawapo eneo la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema jana kuwa tukio hilo ni la Mei 14, mwaka huu saa 1:00 usiku katika eneo la Mawezi , Manispaa ya Morogoro.

Mtuhumiwa alikutwa katika duka la Hadija Hamis (35) mkazi wa Chamwino, wakati alipohitaji kuwekewa fedha hizo, mwenye duka alimtilia shaka hivyo kuarifu Polisi. 

Mtuhumiwa alipokamatwa na askari baada ya kutolewa taarifa Kituo cha Polisi, alikutwa akiwa na noti bandia 87 za Sh 10,000.

Alitaja namba za noti hizo ni BX 7287490 zikiwa noti 22 , BX 728792 zikiwa noti 20, BX 728791 noti 19 na BX7287487 zikiwa noti 15 na kufanya jumla ya thamani ya Sh 870,000 ambazo ni bandia.

Kamanda Matei alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Rashidi Shabani (30) na Michael Lukasa (39), wote wakazi wa Ngerengere wanashikiliwa na Polisi kwa kuwakuta na nyama ya nyati kilo 300 na silaha aina ya gobole iliyotumika kumuulia mnyama huyo.

Kamanda wa Polisi wa Morogoro, Matei, alisema walikamatwa Mei 14, mwaka huu saa 2:00 usiku katika kijiji cha Kinonko, kata ya Gwata, wilaya ya Morogoro. 

Matei alisema, kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jitihada zinazofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kukomesha vitendo vya uhalifu.

I am a

Polisi Akamatwa na Noti Bandia Zenye Thamani ya Sh. 870,000


ASKARI Polisi Ezekiel Dinoso (32) mkazi wa tarafa ya Mgeta, wilayani Mvomero mkoani Morogoro amekutwa na noti bandia za Sh 10,000 zenye thamani ya Sh 870,000, akijiandaa kuzitumbukiza katika akaunti ya mtandao wa Tigo Pesa katika duka mojawapo eneo la Mawenzi, Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, alisema jana kuwa tukio hilo ni la Mei 14, mwaka huu saa 1:00 usiku katika eneo la Mawezi , Manispaa ya Morogoro.

Mtuhumiwa alikutwa katika duka la Hadija Hamis (35) mkazi wa Chamwino, wakati alipohitaji kuwekewa fedha hizo, mwenye duka alimtilia shaka hivyo kuarifu Polisi. 

Mtuhumiwa alipokamatwa na askari baada ya kutolewa taarifa Kituo cha Polisi, alikutwa akiwa na noti bandia 87 za Sh 10,000.

Alitaja namba za noti hizo ni BX 7287490 zikiwa noti 22 , BX 728792 zikiwa noti 20, BX 728791 noti 19 na BX7287487 zikiwa noti 15 na kufanya jumla ya thamani ya Sh 870,000 ambazo ni bandia.

Kamanda Matei alisema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na baada ya uchunguzi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Katika tukio jingine, Rashidi Shabani (30) na Michael Lukasa (39), wote wakazi wa Ngerengere wanashikiliwa na Polisi kwa kuwakuta na nyama ya nyati kilo 300 na silaha aina ya gobole iliyotumika kumuulia mnyama huyo.

Kamanda wa Polisi wa Morogoro, Matei, alisema walikamatwa Mei 14, mwaka huu saa 2:00 usiku katika kijiji cha Kinonko, kata ya Gwata, wilaya ya Morogoro. 

Matei alisema, kukamatwa kwa watuhumiwa hao kumetokana na jitihada zinazofanywa na polisi kwa kushirikiana na wananchi katika kukomesha vitendo vya uhalifu.

I am a

Mganga mbaroni akidaiwa kugoma kumhudumia mjamzito


Polisi mkoani Mara inamshikilia mganga wa zahanati katika Kijiji cha Rwamchanga wilayaniSerengeti kwa madai ya kushindwa kumhudumia mjamzito aliyejifungua pacha na kusababisha kifo cha mtoto mmoja.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ramadhan Ng’anzi alisema tukio hilo lilitokea Mei 15.

“Tunamshikilia kwa makosa matatu, likiwamo la uzembe, kufanya makusudi na kushindwa kuwajibika sawa na kiapo cha kazi yake, tunaendelea na mahojiano yatakapokamilika atafikishwa mahakamani,”alisema Ng’anzi.

Akisimulia chanzo cha mwanae kupoteza maisha, Shida Mugesi akiwa katika Hospitali ya Nyerere alisema alifika zahanati saa 12 asubuhi na kumuomba mganga amuhudumie, lakini alikataa.

“Nilikaa kwa muda wa saa mbili bila kupatiwa huduma, ghafla nilihisi uchungu wa kusukuma mtoto tukamuita mganga wa zamu ili anisaidie aligoma na kudai nimsubiri anakwenda kuoga na wakati huo alikuwa anazungumza kwa simu bila kuonyesha ushirikiano. Nilianza kujifungua mwenyewe,” alisema.

Muuguzi ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema walipopima uzito wa watoto kwa mjamzito huyo walibaini kuwa aliyefariki alikuwa na kilo 2.5 na mwingine 2.3.

Muuguzi wa zahanati hiyo, Frida Kasonga alisema aliposikia taarifa ya kuwapo kwa mgonjwa huyo alilazimika kurudi kituoni kumsaidia lakini alikuta mtoto mmoja ameshafariki dunia.

“Haikuwa zamu yangu ila nililazimika kurudi baada ya kusikia mganga aliyekuwa zamu kagoma kuwasaidia,” alisema Frida.

Ofisa mtendaji kata, Fadhila Nyamburapi na Mwenyekiti wa kitogoji cha Kazi, Samwel Nyakande walilaani kitendo hicho na kutaka sheria ichukue mkondo wake.

Rais Magufuli Atishia Kuwatumbua JIPU Mawaziri Wawili......Wenzao Wabaki Vinywa Wazi Kikaoni

Operesheni ya kutumbua majipu ya Rais John Magufuli nusura iwaangukie Mawaziri wawili ambao  pia walikuwa  manaibu  mawaziri katika Serikali ya Awamu ya Nne.

Taarifa kutoka katika chanzo cha kuaminiwa zimeeleza kuwa Rais Magufuli alionesha kutoridhishwa na utendaji wa Mawaziri hao na kuwafokea mbele ya mawaziri wenzao  kwa kuwataja majina katika kikao maalum cha mawaziri kilichofanyika hivi karibuni.

"Ni mazingira ambayo mawaziri hawakuyazoea kwamba Rais anawaambia moja kwa moja kwa majina, anafoka akisema anaweza kuwafukuza wakati wowote.....

"Mawaziri wamezoea mara kwa mara wanapofanya kosa au uzembe wanaonywa kwa staili tofauti, ni kama ya kistaarabu hivi. Sasa huyu bwana mkubwa hana mchezo, aliwataja kabisa, tena mbele ya wenzao ambao walibaki vinywa wazi.

“Wewe (anataja jina la Waziri) na mwenzako (anamtaja jina pia) nitawatumbua,” Chanzo cha gazeti la Rais Mwema kinamkariri Rais Magufuli.

Mawaziri hao ambao ni wabunge wa kuchaguliwa majimboni kwa upande wa Tanzania Bara, wanaongoza wizara nyeti ambazo zinasimamia sekta mtambuka, wizara ambazo zinagusa sehemu ya ahadi za mabadiliko alizonadi Magufuli wakati akigombea urais katika kampeni za mwaka jana.

Chanzo hicho kilieleza kuwa Rais Magufuli aliwaonya pia mawaziri wengine ambao alionesha kutoridhishwa na utendaji wao kwakuwa hawaendani na kasi yake ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Magufuli alitaka atoe mfano kwa mawaziri wengine kwamba wao si watu maalum sana. Kama wanavyotumbuliwa watu wengine na wao pia wanaweza kutumbuliwa,” kiliongeza chanzo hicho

Rais Magufuli aliunda Baraza lake la Mawaziri mwishoni mwa mwaka jana na kuwashauri wasifanye sherehe ya kuteuliwa kwakuwa wakifanya vibaya hatawaonea haya atawaondoa mara moja bila kujali majina yao.

Utendaji wa Rais Magufuli umeendelea kusifiwa kila kona hususan katika kuwawajibisha viongozi wa ngazi zote na kuonesha nia ya dhati ya kuwahudumia watanzania huku akipambana na uzembe na ufisadi.

Saturday, 14 May 2016

Ahukumiwa Kifungo cha Miaka 30 Jela Kwa Kumuoa Bunti Yake wa Kumzaa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma, jana ilimhukumu kifungo cha miaka 30, Godfrey Mjelwa (48), baada ya kupatikana na hatia ya kuishi kinyumba na binti yake wa kumzaa.

Hakimu Mkazi katika mahakama hiyo, Mwajuma Lukindo alisema ushahidi wa pande zote ulithibitisha kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo la kuishi chumba kimoja na binti yake, kama mke na mume.

Kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa, Mjelwa aliamua binti yake mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa) kuwa mke na kuishi naye katika Mtaa wa Kizota Manispaa ya Dodoma. 

Hakimu Lukindo alisema kosa alilokutwa nalo mtuhumiwa ni ‘maharimu’ (kufanya mapenzi na ndugu za damu), licha ya kuwa mtoto huyo bado alikuwa mdogo, lakini ni mtoto wake wa kumzaa.

Mwendesha mashtaka Janeth Mgome, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa, ili liwe fundisho kwa wengine ambao wana tabia ya aina hiyo. 

Utetezi wa mtuhumiwa huyo uliwavunja mbavu watu waliokuwapo mahakamani hapo, kwani alitaka kupunguziwa adhabu kwa kuwa mtoto wake ana miaka 14 na miezi tisa na siku tisa, siyo miaka 15 kama ilivyodaiwa mahakamani hapo.

Lady Jaydee Amtaka Gardner Aombe Radhi Ndani ya Siku 7


Msanii wa muziki Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ kupitia mwanasheria wake Aman G. Tenga kutoka Law Associates (Advocate) ameandika barua ya kumtaka mtangazaji maarufu wa Clouds Fm, Gardner G. Habash, kuomba msamaha mbele ya umma kutokana na kauli yake ya uzalilishaji aliyoitoa dhidi yake.

Gardner ambaye alikuwa mume wa muimbaji huyo wa Ndindindi, anatuhumiwa kulifanya kosa hilo mnamo tarehe 6 May 2016, akiwa kama mshereheshaji tamasha la Miss TIA 2016 lililofanyika CDS Park (zamani TCC) ambapo alidaiwa kutamka kwa makusudi maneno ya udhalilishaji na kejeli“Nimeshamkojoza kwa miaka kama 15 hivi” mbele ya umma.

Baada ya wiki moja toka tukio hilo litokea, Lady Jaydee kupitia mwanasheria wake ameandika barua hii.

  

Wednesday, 11 May 2016

Bomu la Mkono Laibua Hofu Tanga.....Ni baada ya Mtuhumiwa Kulirusha Baada ya Kukurupushwa na Polisi

Kwa mara nyingine jana wakazi wa Jiji la Tanga walikumbwa na taharuki baada ya kijana mmoja kurusha bomu la mkono chini ya daraja wakati wananchi walipokuwa wakimfukuza baada ya kukurupushwa na polisi.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Leonard Paulo alisema kijana huyo alikurupushwa na askari waliokuwa kwenye msako wa kuwatafuta majambazi waliofanya mauaji Aprili 20, mwaka huu katika duka la Central Bakery.

Alisema tukio hilo lilitokea juzi saa mbili usiku kwenye Mtaa wa Makora, Tarafa ya Ngamiani.

Awali, Kamanda Paulo alisema kijana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka kati ya 25 na 30, alipokurupushwa alianza kutimua mbio. 

“Alipoanza kukimbia ndipo wananchi wakaingilia kati, walimfukuza na kumshambulia kwa mawe huku wakimpiga na kitu chenye ncha kali kisogoni, ndipo wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo akafariki dunia njiani,” alisema Kamanda Paulo.

Mapema kabla hajafariki dunia, kamanda alisema kijana huyo alipokurupushwa alikimbia akiwa ameshikilia bomu mkononi.

Kamanda aliwataka wakazi wa Tanga kuwa watulivu kwa sababu vyombo vya dola viko katika operesheni maalumu ya kuwasaka walioshiriki mauaji ya hivi karibuni katika hilo la mikate.

Walioshuhuda tukio hilo walisema kijana huyo alishambuliwa na wananchi baada ya kukwapua simu ya mwanamke mmoja katika Mtaa wa Makorora.

Rais Magufuli: Huyu Shetani Aliyetulaani Watanzania kwanini Asife? Hivi Hatuhurumii hata Kidogo?

SHIRIKA la Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF) limetakiwa kuingia ubia na kampuni za madini nchini ili kutengeneza ajira kwa vijana wa Kitanzania ambao wengi wao wako vijiweni.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Rais John Magufuli wakati akizindua majengo ya mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF yaliyogharimu zaidi ya Sh bilioni 60 yaliyojengwa jijini hapa.

Rais Magufuli alisema wakati umefika kwa NSSF kujikita katika biashara ya kupata faida kwa haraka kama vile ya madini ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kukata madini hayo na kusanifu ili vijana wafundishwe na hatimaye kuajiriwa katika viwanda hivyo.

Alisema suala la Tanzania kuwa nchi ya tatu duniani kwa kuuza madini ya tanzanite wakati madini hayo yanapatikana hapa hapa tu na kuziacha nchi za India na Kenya zikiongoza, ni suala la kushangaza sana.

Alisema NSSF sasa inapaswa kujipanga na kuingia katika biashara ya madini hususan tanzanite kwa kuingia ubia na kampuni kama hiyo ya Signature inayomilikiwa na mzawa Sailesh Pandit ili ifanye biashara na wanachama wa mfuko huo wapate faida haraka haraka na kuachana na uwekezaji wa majengo.

"Siku nyingine hakuna ubaya hata NSSF mkawa ndio wawekezaji wakubwa wa Tanzanite mkawa mnanunua Tanzanite kutoka kwa vijana hawa badala ya kuwa inavushwa mpaka Kenya na kwenda Kenya, badala ya Tanzania kuwa ya kwanza kuuza Tanzanite duniani inajitokeza India alafu inafata Kenya

"Unajua saa nyingine watu wanatuona Watanzania sijui tukoje, huyu shetani aliyetulaani sisi Watanzania kwanini asife? hata hatuhurumii kidogo? basi kama ni kuswali na kusali tusali sana ili tubadilike, tuthamini mali yetu kwa ajili ya vizazi vyetu." Alisema RAais Magufuli

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Profesa Godius Kahyarara alisema kampuni ya madini ya Signature iliyopanga katika jengo la mfuko huo la Mafao House imeajiri vijana zaidi ya 47 wa kuchonga tanzanite na watashirikiana katika kuanza biashara hiyo.

Profesa Kahyarara alisema kauli ya Rais ya shirika hilo kujikitaka katika biashara ya tanzanite kwa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo wataifanyia kazi haraka iwezekanavyo bila ya wasiwasi wowote.

Hata hivyo, serikali ilishapiga marufuku usafirishaji wa madini ghafi nje ya nchi na kutaka madini yote kuchongwa nchini na wazawa kuanzisha viwanda vya kuchonga madini hayo.

Polisi Mwanza Yanasa Mtandao wa Ujambazi

Polisi mkoani Mwanza imebaini mtandao unaohusika na ujambazi wa kuvamia, kupora, kujeruhi na kuua wafanyabiashara wa maduka ya fedha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema tayari wamewatia mbaroni watu watatu wanaodaiwa kuhusika na mtandao huo wakiwa na bunduki aina ya SMG ikiwa na magazine nne na risasi 144.

Pia, watuhumiwa hao walikutwa na kofia moja ya kuficha uso, hijabu mbili, jaketi moja pamoja na mabegi mawili wanayotunzia silaha zilizokuwa zimefichwa kwenye nyumba wanayoishi.

“Polisi bado inaendelea kumsaka kinara wa mtandao huu (jina linahifadhiwa), ambaye alifanikiwa kukwepa mtego wa polisi, tunawaomba raia wema kutoa taarifa zitakazofanikisha kumtia mbaroni,”alisema SACP Msangi.

Alisema bunduki iliyokamatwa inaaminika kutumika katika matukio zaidi ya sita ya uporaji katika maduka ya fedha.

Hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga alisema vyombo vya dola tayari vimebaini mitandao saba ya uhalifu mkoani Mwanza.

Kitwanga ambaye pia ni mbunge wa Misungwi aliwaeleza wapigakura wake kuwa tayari mitandao miwili kati ya hiyo saba ilikuwa imeangamizwa, huku jitihada za kuangamiza iliyosalia zikiendelea.

Monday, 9 May 2016

Vigogo Chadema Kyela Wavuliwa Uongozi kwa Usaliti

Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, Saadati Mwambungu pamoja na wajumbe 19 wa kamati ya utendaji wa wilaya hiyo, wamevuliwa uongozi baada ya kutuhumiwa kukihujumu chama.

Hatua hiyo ilifikiwa juzi jioni na uongozi wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, chini ya mwenyekiti wake, Dk Stephen Kimondo na Mratibu wa Kanda, Frank Mwaisumbe na kuweka wilaya hiyo chini ya uangalizi wa uongozi wa Mkoa wa Mbeya ndani ya siku 30 wakati wakiendelea na uchunguzi.

Mratibu wa Chadema katika Kanda hiyo, Frank Mwaisumbe alisema jana kuwa baada ya kufanyia kazi tuhuma 17 zilizowasilishwa kwao na wanachama wa chama hicho wilaya, walibaini kuwa tuhuma saba kati yake zina ukweli dhidi ya viongozi hao hivyo wakafikia uamuzi wa kuwasimamisha na kuwataka kurudisha mali zote za chama hicho ndani ya siku 30.

“Ni kweli jana (juzi) tulifika Kyela na katika kikao chetu na kamati ya utendaji ya wilaya tulipowahoji ilionekana tuhuma saba zina ukweli na baadhi ya watuhumiwa walikiri. Miongoni mwa tuhuma hizo ni matumizi mabaya ya fedha na mali za chama, kutoshiriki vyema Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana hadi tukapoteza jimbo, hususani siku ya kuhesabu kura za jumla viongozi walikimbia.

“Siku ile ya uchaguzi wa mwaka jana kuna vijana wetu walikamatwa wakituhumiwa kuvunja ofisi pale halmashauri ya Kyela na wakahukumiwa, lakini hakuna kiongozi yeyote ngazi ya wilaya aliyethubutu hata kwenda kuwaona pale gerezani hadi walipojinasua wenyewe,” alisema Mwaisumbe.

Alisema kutokana na mkutano wao wa juzi wajumbe wake kutotimia ili kufikia uamuzi halali wa kuwachukulia hatua zaidi, uongozi wa Kanda uliamua kuwasimamisha na chama kuwa chini ya mkoa, huku ukifanyika utaratibu wa kuitisha mkutano mkuu ambao utawajadili kwa kina na kuona kama watafukuzwa moja kwa moja au la.

Mwambungu alipoulizwa juu ya kutimuliwa kwao, alikiri huku akisisitiza kwamba tuhuma zilizotolewa hazina ukweli wowote kikatiba, na badala yake zimetengenezwa na ‘genge’ la watu wachache kwa uchu wa madaraka, lakini hana kinyongo kusimamishwa uongozi kwa kuwa ipo kikatiba ndani ya Chadema.

Alisema; “Kwanza ni heshima kwa kuwa jambo hili lipo kikatiba. Lakini katika mkutano wa juzi akidi ya wajumbe haikutimia kwani Chadema Wilaya ya Kyela ina wajumbe 349 wa mkutano mkuu, lakini kwa juzi wajumbe waliohudhuria walikuwa 120 tu.

“Ndiyo maana uongozi wa Kanda ulitoa siku 30 za kufanyika mkutano mkuu utakaowajumuisha wajumbe wote 349 na ndipo itakapofahamika… kama ni kufukuzwa au kuendelea na uongozi,”alisema.

Mwambungu alisema kati ya wajumbe 19 wa kamati ya utendaji ya wilaya, wajumbe saba waliamua kujiuzulu uongozi na baadaye wakaungana na wengine ambao waliunda tuhuma hizo kwa lengo na kuuangusha uongozi ikiwa ni maandalizi ya uchaguzi mwaka 2020.

Saturday, 7 May 2016

Wakurugenzi Katavi Kikaangoni ......Mkuu wa Mkoa Awataka Warejeshe Milioni 200 Walizolipa Watumishi Hewa

Wakurugenzi wa Halmashauri zote mkoani Katavi, wameagizwa kurejesha Sh200 milioni wanazodaiwa kuwalipa watumishi hewa ndani ya siku 21.

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja Jenerali mstaafu, Raphael Muhuga alitoa agizo hilo jana katika kikao baina yake na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa pamoja na waandishi wa habari.

Alikuwa akitoa taarifa ya kubainika kwa watumishi hewa wapya mkoani humo.

Muhuga alisema kuendelea kubainika kwa watumishi hao hewa, itawabidi wakurugenzi kuhakikisha fedha zote zilizolipwa kwa watu hao zinarejeshwa serikalini kwa muda aliowataka wazirejeshe na wampatie taarifa itakayothibitisha fedha hizo kurejeshwa.

Pia, mkuu huyo wa mkoa aliagiza maofisi wa ofisi ya utumishi wachukuliwe hatua ya kinidhamu kwa kusababisha watumishi hao hewa kulipwa fedha.

“Hili siyo suala la bahati mbaya, bali hawa watu walidhamiria kulipa mishahara hiyo hewa naimani wapo wenye maslahi juu ya jambo hili,”alisema Muhuga.

Aliagiza wakurugenzi wote wa halmashauri, wahakikishe maofisa utumishi wanawafuta watumishi hewa wote kwenye leja zao na wawachukulie hatua wote waliohusika na suala hilo.

Hata hivyo, aliishukuru kamati ya watu wanne iliyoundwa kufanya kazi ya uhakiki wa watumishi mkoani humo.

Aliitaka iharakishe kukamilisha uchunguzi wa watumishi 15 ambao taarifa zao zimebainika kuwa na utata.

Ahukumiwa Miaka Mitatu Kwa Kosa la Kumtukana Mtandaoni Mwanamke Aliyedai Anatembea na Mumewe


Mfanyabiashara Naila Aminel (24) amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni tano baada ya kukiri kutumia mtandao wa kompyuta kutuma ujumbe wa lugha ya matusi.

Aminel ambaye ni mkazi wa Kariakoo, alihukumiwa kifungo hicho jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Said Mkasiwa.

Awali, akisoma mashitaka, Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Februari 13 mwaka huu, maeneo ya katikati ya jiji, wilayani Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Mitanto alidai kuwa mshitakiwa alitumia lugha ya matusi dhidi ya Martha Sebarua kupitia mtandao wa kompyuta kinyume na kifungu namba 23 (1) na (3) cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.

Hata hivyo, Mitanto aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo.

Mshitakiwa huyo alidai hakumtukana mlalamikaji isipokuwa alifanya hivyo kwa kuwa alimchukulia mume wake na walipiga picha za utupu na kumtumia kwenye simu yake.

Aliiomba pia mahakama kumpunguzia adhabu kwa kuwa ana watoto wadogo ambao wanamtegemea.

Hakimu Mkasiwa alisema kuwa mshitakiwa amekiri kutumia lugha ya matusi hafai katika jamii na kwa sababu kosa lake ni la kwanza, atatakiwa kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni tano

Ushahidi wa Mwalimu Kupigwa Kofi na Afisa Elimu Watua Kwa Mkuu wa Wilaya

CHAMA cha Walimu (CWT) Rukwa, kimemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Mathew Sedoyeka ushahidi wa maandishi unaoelezea kitendo cha Ofisa Elimu, Shule za Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga, Peter Fusi, kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani.

 

Ushahidi huo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya na Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Rukwa, Hance Mwasajone.

 

Ushahidi huo wa kimaandishi wa tukio hilo umeandikwa na mwalimu mwenyewe, Jacob Msengezi (25) ambaye alisema alipigwa mbele ya wanafunzi wake akiwa darasani shule ya msingi Kianda kabla ya kuamuru walimu wengine kufanya usafi kwa kuokota mbigili ‘miba’ iliyotapakaa katika eneo la shule hiyo akidai kuwa huo ni uchafu.

 

Sedoyeka aliwaruhusu viongozi hao kumtembelea mwalimu na kusisitiza kuwa anafuatilia kwa karibu mkasa huo ili sheria ichukue mkondo wake

Friday, 6 May 2016

Walimu Wagoma, kisa mwenzao kuzabwa kofi darasani na Ofisa Elimu

WALIMU wa shule ya msingi Kianda wameanza mgomo wa siku mbili wa kutofundisha shuleni hapo huku wakilaani kitendo cha Ofisa Elimu (Shule za Msingi) wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, Peter Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao akiwa darasani mbele ya wanafunzi wake.

Makamu Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Flora Kipesha alisema wameitisha mgomo huo wa siku mbili kupinga kitendo cha Fusi kumshambulia na kumpiga makofi mwalimu mwenzao Jacob Msengezi (25) ambaye anafundisha somo la Hisabati Darasa la Saba shuleni hapo.

“Licha ya kulaani vikali kitendo hiki cha udhalilishaji alichofanyiwa mwalimu mwenzetu na Ofisa Elimu (DEO) wetu (Peter Fusi) kumcharaza makofi mbele ya wanafunzi wake akiwa darasani ….Ametudhalilisha sote yaani hata hamasa ya kufundisha imetoweka ….. 

“Sasa hatutaingia darasani kufundisha kwa siku mbili tukimshinikiza Mkurugenzi wa Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga (Adam Missana) achukue hatua dhidi ya ofisa huyo wa elimu ……yaani tunadhalilishwa hivi mbele ya wanafunzi wetu wenyewe wakati kazi hii tumeisomea na tuna vyeti halali ….Tukiwa na sifa stahiki za taaluma ya ualimu,” alieleza Kipesha. 

Akifafanua, alisema walimu hawataingia kufundisha kwa siku hizo mbili na watakuwa ofisini wakiandaa mitihani huku wanafunzi wakiendelea kuhudhuria shuleni hapo kama kawaida.

Mwalimu Msengezi alisema tukio hilo lilitokea Jumatano saa tatu asubuhi shuleni hapo baada ya ofisa elimu huyo kufanya ziara ya kikazi. 

“Nilikuwa na kipindi cha somo la hesabu kuanzia saa mbili hadi saa 2.40 asubuhi kwa kuwa mwalimu wa somo la Kiingereza alikuwa ‘busy’ niliamua kubakia darasani humo nikisahihisha madaftari ya wanafunzi wangu, ndipo nikamwona akiwa eneo la shule, hivyo nikaamua kwenda ofisini kujiandaa na ukaguzi,” alisema.

Aliongeza kuwa, “Wakati nikiwa ofisini aliingia chumba cha darasa la saba na kukuta wanafunzi wakiwa pekee yao, ndipo alipoamuru aitwe mwalimu aliyekuwa akifundisha darasa hilo. 

“Nilikwenda darasani na kukutana naye, nilimweleza ilivyokuwa, basi akaniuliza kwani sasa ni saa ngapi? 

"Nilipomjibu kuwa ni saa tatu asubuhi alighadhabika na kunipiga makofi. Nilipohisi anajiandaa kuniadhibu zaidi nilitimua mbio na kutoka darasani,”alisema mwalimu huyo. 

Aliongeza kuwa tayari ameshafikisha malalamiko yake kwa Katibu wa Chama cha Walimu nchini (CWT) Wilaya ya Sumbawanga Vijijini, Vicent Ndewele kwa hatua zaidi. 

Ndewele amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akiahidi kuwa chama hicho kitatoa msimamo wake kwa vyombo vya habari.

FUNDI MITAMBO WA REDIO BOMBA FM 104.0 MBEYA ATISHIA KUJIRUSHA TOKA MNARANI KWA MADAI YA KUDAI MSHAHARA WAKE

Fundi Mitambo wa Redio Bomba Fm 104.0 iliyopo Jijini Mbeya Jina lake Limehifadhiwa alileta tafrani Mchana wa Leo mara baada ya kupanda juu ya  mtambo wa Redio hiyo, na kutishia kujitupa chini kwa madai ya kuhitaji kulipwa mshahara wake kutoka kwa muajiri wake wa kituo hicho cha Redio kilichopo maeneo ya Block "T" Jijini Mbeya.

Fundi Mitambo wa Redio Bomba Fm (jina kapuni) akiwa juu ya Mnara wa Redio hiyo huku akisikika kusema "Mpaka Kieleweke leo nataka Pesa Zangu..."

Mpaka Kieleweke...

Baadhi ya wakazi na Wananchi wa Jiji la Mbeya wakishuhudia tukio hilo...

                                    KWA HISANI YA  MR.PENGO MMG MBEYA

MKUU WA MKOA WA MBEYA AZINDUWA RASMI MASHINDANO YA UMISETA LEO JIJINI MBEYA YANAYODHAMINIWA NA COCACOLA..

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla akisalimiana na baadhi ya Wachezaji wa Timu za Shule za Sekondari zilizo shiliki katika Uzinduzi huo wa Mashindano ya Umiseta kwa Shule za Sekondari Mkoa wa Mbeya, ambapo Shule zote zilizo Shiriki katika Mashindano hayo Yanayotarajia kuanza hivi Karibuni katika Viwanja Mbalimbali Mkoani hapo walipewa Zawadi ya Vifaa vya Michezo kwa kila Shule iliyo Shiriki Sambamba na Vinywaji kutoka katika Kampuni ya Kuzalisha Vinywaji vya Soda Cocacola Ambao ndio Wadhamini Wakuu wa Mashindano hayo ya Umiseta Mwaka huu.

Kikundi cha Waburudishaji Jijini Mbeya kikitoa Burudani katika Uzinduzi huo wa Mashindano ya Umiseta Mwaka 2016 ulio fanyika katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Baadhi ya Wanamichezo kutoka Shule za Sekondari Jijini Mbeya wakionyesha Umahiri wao katika Michezo...

Mmoja kati ya Wanafunzi akipewa Huduma ya Kwanza kutoka kwa Wanafunzi wenzake Mara baada ya kupoteza Fahamu kwa kukosa Hewa katika Hafra hiyo iliyofanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu Sokoine Jijini Mbeya.

Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria Hafra hiyo ya Uzinduzi wa Mashindano ya Umiseta uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

PICHA ZOTE KWA HISANI YA MR.PENGO MMG MBEYA.

Tuesday, 3 May 2016

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu Atoa ONYO Kali kwa Wanaume Wanaowapa Mimba Wanafunzi


Serikali imewaagiza Maafisa maendeleo ya Jamii na maafisa ustawi wa Jamii wa wilaya,kata na mikoa nchini kuwafatilia wanaume wanaowapa ujauzito watoto wa shule na kuwafikisha Mahakamani.

Akizungumza leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, amesema serikali haitamvumilia mwanaume yoyote anaempa mwanafunzi ujauzito.

Mhe. Ummy amesema kuwa serikali ya awamu ya tano itawachukulia hatua wanaume wote na hakutakuwa na huruma juu ya hilo huku akisisitiza wanawake ambao si wanafunzi ni wengi mitaani.

Hapo awali Akijibu Swali la Mbunge wa Ileje, Mhe. Janeth Mbene, Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema kuwa tatizo la watoto kupewa ujauzito nchini linatokana na vishawishi wanavyokutana wakiwa njiani wakati wanakwenda mashuleni.

Sumaye Ampiga Kijembe Rais Magufuli


FREDERICK Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu ameeleza kushangazwa na Serikali ya Rais John Magufuli kupenda kusifiwa zaidi na kuchukia kukosolewa

Sumaye bila kumtaja jina Rais Magufuli ameleza kushangazwa na hatua ya serikali kuminya uhuru wa habari na kwamba, kufanya hivyo kunalenga kuficha madudu yanayofanywa na watendaji wake.

“Wapowatawala ambao hawapendi kusemwa lakini wanapenda sana kusifiwa. Kiongozi mwenye tabia ya udikteta hataki kusikia kingine zaidi ya sifa zake tu.

“Huyo ni mtu hatari na katika nchi ya namna hiyo hakuna uhuru wa habari wala uhuru wa kutoa maoni kwa woga wa kupotezwa kusikojulikana,”amesema Sumaye.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliyoratibiwa na Chama cha Waandishi wa Habri za Siasa (TAPOREA), Sumaye amesema, serikali inakiuka Katiba ya nchi.

Amesema, serikali yoyote inayopambana na vyombo vya habari na kuminya uhuru wa kufanya kazi zao huwa ina tatizo kwa upande wa wanaotawala.

Akitolea mfano wa hatua ya serikali kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya bunge Sumaye amesema, kwa kufanya hivyo serikali imevunja Katiba.

“Unapoondoa matangazo ya moja kwa moja ya vipindi vya Bunge, kwanza ni kuvunja katiba. Ibara ya 18 (d) ya Katiba inasema, kila mtu ana haki ya kupewa taarifa wakati wote.

“Kwa kuzuia Bunge kuoneshwa ‘live’ (moja kwa moja) wewe serikali unataka kutoa taarifa ya Bunge kwa wakati unaoutaka na kwa taarifa unayoitaka wewe,” ameeleza Sumaye.

Kuhusu sababu iliyotolewa kwamba, matangazo hayo yanatumia gharama ya Sh. 4 bilioni amesema haina mashiko.

Sumaye amesema, hata kama matangazo hayo yatarushwa na ofisi za bunge bado, gharama zitaongezeka zaidi kwa sababu Bunge litahitaji kununua mitambo pamoja na kuajiri wafanyakazi wake.

Sumaye amesema, serikali yenye demokrasia ya kweli lazima ikubali wananchi wake kutoa maoni.

“Serikali yoyote yenye utawala bora, ingependa mambo yake inayoyafanya kwa ajili ya wananchi wake mambo hayo yajulikane kwa wananchi hao.

“Ukiona serikali inaficha mambo yake lazima kuna mambo wanayoyafanya ambayo hayafai na wasingependa jamii ijue,” amesema Sumaye.

George Maziku, Mkurugenzi Mtendaji wa TAPOREA amezungumzia ripoti ya hali ya uhuru wa waandishi wa habari na uhuru wa vyombo vya habari kimataifa, iliyotolewa na Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka lenye Makao Makuu yake nchini Ufaransa haipendezi.

Amesema, ripoti hiyo inaonesha kuwa, katika miaka 10 iliyopita zaidi ya waandishi wa habari 800 kutoka mataifa mabalimbali duniani wameuawa wakiwa wanatekeleza kazi zao.

“Kitisho kingine kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini ni utamaduni mpya ulioasisiwa na kuimarishwa na watawala wa sasa na kuvishinikiza vyombo vya habari kutomkosoa Rais John Magufuli na serikali yake.

“Matokeo yake, vyombo vingi vya habari nchini vimelazimika kuandika habari za kumfurahisha Rais Magufuli,” amesema Maziku.

Monday, 2 May 2016

Watahiniwa 75,000 Waanza Mtihani wa Kidato cha Sita Leo


Watahiniwa  74,920 leo wanaanza kufanya mtihani wa kuhitimu Kidato cha Sita katika shule mbalimbali nchini huku watahiniwa 11,597 wakifanya mtihani wa Ualimu.

Ofisa Habari wa Baraza la Mitihani (NECTA), John Nchimbi amesema kuwa mtihani wa kidato cha sita unaanza leo hadi Mei 19, mwaka huu. 

Nchimbi amesema kati ya watahiniwa hao waliosajiliwa, watahiniwa 65,610 ni watahiniwa wa Shule huku watahiniwa wa Kujitegemea wakiwa 9,310.

“Kati ya watahiniwa wa shule 65, 610, watahiniwa wasichana ni 24,549 na wavulana ni 41,061 huku watahiniwa wa kujitegemea wasichana wakiwa ni 3,176 na wavulana ni 6,134,” alisema Nchimbi.

Kwa upande wa mtihani wa ualimu, Nchimbi amesema kati ya watahiniwa 11,597 watakaofanya, watahiniwa 10,942 wanafanya Ualimu Daraja A na watahiniwa 654 wanafanya mtihani wa Stashahada ya Sekondari na mmoja anafanya Stashahada ya Ufundi.

“NECTA inatoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa, na wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mazingira ya vituo vya mitihani yapo salama, tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu. 

“Kwa wanafunzi tunaamini walimu wamewaandaa vizuri, na ni matarajio yetu wanafunzi watafanya mitihani yao kwa kuzingatia taratibu zote za mitihani ili matokeo ya mitihani yaoneshe uwezo wao halisi kulingana na maarifa na ujuzi waliopata katika kipindi walipokuwa shule,” aliongeza Nchimbi.

Aidha, Nchimbi alitoa mwito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa kuhakikisha mtihani unafanyika kwa amani na utulivu na kusisitiza kuwa mtu asiyehusika na mtihani asiingie kwenye eneo la mtihani.