Mchungaji
wa kanisa la huduma katika roho wilayani Karagwe, Jafece Josephat
anashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kumuoa mke wa
muumini wake na kuanza kuishi naye kama mke na mume akidai ameoteshwa na
Mungu.
Mchungaji huyo amekamatwa jana baada ya kamati ya ulinzi na usalama na kamati ya amani na maadili ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo, Godfrey Mheruka kufika kanisani hapo na kupata ukweli juu ya jambo hilo baada ya pande zote akiwemo mchungaji wa kanisa Josephat, mwanamke aliyefahamika kwa jina la Domina Damian na mme wake wa mwanzo Donath Appolo kueleza ukweli jinsi walivyooteshwa mpaka hatua ya mke kuolewa.
Mkuu wa Wilaya Akimhoji Mchungaji
Mkuu wa Wilaya akimhoji mume wa huyo mwanamke
==>Huyu ndo mke wa mtu alieolewa na mchungaji
Mheruka
alitoa agizo la kukamatwa kwa mchungaji huyo kutokana na baba wa
Appolo aliyenyang'anywa mke kujitokeza mbele ya kanisa hilo na kudai
mahari aliyomtolea mtoto wake irudishwe kwani hawezi kuutolea mahari
ukoo mwingine kwa kuwa mke ameshaolewa na mme mwingine.
"Kwa
kuwa, mke ameacha familia yake akaja kuolewa na wewe mchungaji amezini
na kwa kuwa wewe unayejiita mchungaji umeiacha familia yako ya watoto
watano ukaoa mke mwingine nyote mnazini kwani kinachotenganisha ndoa ya
mke na mme ni kifo lakini nyie mmejichukulia maamuzi yenu binafsi,"amesema Mheruka.
Mheruka
amemwagiza mwangalizi wa kanisa hilo kuendelea kutoa huduma katika
kanisa hilo ndani ya miezi sita huku akitafuta utaratibu wa mchungaji
mwingine mwenye maadili mema na kuwa wao kama Serikali watachunguza
vizuri kama kanisa hilo limesajiliwa au halijasajiliwa ili hatua zaidi
ziweze kuchukuliwa.
No comments:
Post a Comment