Hakimu
Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu Cyprian Mkeha amemuuliza mfanyabiashara
Yusufu Manji kwa nini amechelewa mahakamani wakati walipaswa kuanza saa
tatu asubuhi.
Kutokana
na swali hilo, Manji aliomba msamaha kwa kuchelewa na kwamba alipitia
hospitali kabla na aliwasiliana na wakili wake alimueleza kuwa hakimu
yupo kwenye kikao.
Swali
hilo lilikuja baada ya kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin
inayomkabili Manji kushindwa kuendelea na kupelekwa hadi Septemba 25,
2017.
Ni
baada ya Wakili wa Manji, Hajra Mungula leo Jumatatu kueleza kuwa kesi
hiyo ilipangwa kwa ajili kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande
wa utetezi na kwamba wapo tayari.
Wakili
wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis alieleza kuwa yeye anataka kusafiri
mchana na kwa kuwa kesi imechelewa kuanza kusikilizwa hawezi kuendelea.
Hakimu
Mkeha naye alisema anaenda katika kikao mchana huo, hivyo Wakili
Mungula aliomba kesi hiyo ipangiwe siku tatu mfululizo, kwa ajili ya
kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa upande wa utetezi Septemba 25, 26
na 27, 2017.
Upande
wa mashtaka katika kesi hiyo awali walidai watawaita mashahidi
wasiozidi 10 kutoa ushahidi katika kesi hiyo lakini wakatoa watatu na
kufunga ushahidi wao.
Manji
yeye anatarajia kuwaita mashahidi 15 na ametoa mmoja ambaye ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Manji
alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Februari 16, 2017 ambapo
anadaiwa kuwa , kati ya Februari 6 na 9, 2017 katika eneo la Upanga
Sea View Ilala alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin.
No comments:
Post a Comment