Monday 18 September 2017

KIMONDO 101955 BENNU


Mwaka 1930 wanasayansi walikigundua Kimondo chenye ukubwa wa tani 16 ( metric tons ) jijini Mbeya katika wilaya ya Mbozi. Kimondo hicho ni moja ya vimondo maarufu sana duniani kwa ukubwa na uzito vilivyopata kuanguka na kugusa uso wa dunia.
Kijiografia vimondo vingi vilivyopo angani ( outer space ) vimetoka kwenye jua . Joto kali kwenye jua husababisha mawe kutoka kwenye mzingo wake nakushuka chini . Mengi yao hukutana na ukanda wa baridi kali na kuganda na mwisho wa siku kuyeyuka bila kuleta madhara kwenye sayari zinazolizunguka jua ikiwemo dunia yetu. Bila ukanda huo wenye baridi kali sana ( coldest layer ) basi mawe hayo ya moto yangeleta athari kubwa sana .
Vimondo vingi ( asteroids ) vipo kati ya Sayari ya Jupita na Mars. Hapo zimetengeneza mkanda ambao kijiografia unaitwa ' main asteroids belt'. Na vingine hupenya zaidi kusogea kwenye ukanda wa ndani kwenye usawa wa Sayari tatu za mwanzo kwenye mfumo wa jua ikiwemo dunia . Hapo ndipo tunakikiuta kimondo 101955 Bennu ambacho kiligunduliwa na wanasayansi mwaka 1999.

Nilianza kukielezea kimondo maarufu cha Mbozi ili tufahamu kuwa vipo vimondo ambavyo hufanikiwa kupenya ukanda wa baridi kali na kuja kwenye uso wa dunia (ardhi ) kama ilivyotokea kwa kimondo cha Mbozi. Kimondo cha Mbozi si kwamba kilianguka mwaka 1930 bali ni miaka mingi nyuma lakini rekodi yake kisayansi ilifanyika mwaka huo.
Bennu ni aina za vimondo vilivyopo kwenye kundi la vimondo vyenye wingi wa kaboni ( a carbonaceous asteroid ). Ni jamii ya vimondo chini ya kundi kubwa la Appolo ( waliosoma jiografi au watafiti wananielewa hapo ) .
Kimondo hiki au jiwe hili kubwa ambalo linaelezwa ifikapo mwaka 2169 litaigonga dunia na kuifanya ilipuke mithili ya pigo la bomu la Atomic lenye tani 12000 licha ya kugunduliwa mwaka 1999 lakini kitaalamu lilifanyika miaka milioni 10 baada ya kuumbwa au kufanyika kwa mfumo wa jua zaidi ya miaka bilioni 4.6 iliyopita.
Mpaka sasa kuna nadharia mbili juu ya kimondo 101955 Bennu ambacho kimejitengenezea njia ambayo mzunguko wake ifikapo mwaka 2169 huenda ukaingilia njia ya dunia kulizunguka jua na kutokana na ukubwa wake, utaigonga dunia na kuilipua kutokana na nguvu na kasi yake. Nadharia ya kwanza inasema Bennu ilifanyika baada ya kupasuka kwa nyota mbalimbali kwenye makundi ya ' Red giants ' na ' Supernovae '. Vumbi lao , mawe , madini na takataka zingine ndio zilizofanyika mabadiliko mengine ya kikemia na kiumbo na kutengeneza jiwe hilo kubwa lijulikanalo kama Bennu. Lakini pia nadharia ya pili inasema Bennu pia ilifanyika wakati mfumo wa jua ukifanyika miaka bilioni 4.6 iliyopita.
Mgongano huo unatazamiwa kijiografia ndio ukawa mwisho wa Sayari hii iitwayo dunia kwenye mfumo wa jua ingawa maisha ya mfumo huo bado yanakadiriwa kuendelea kwa miaka bilioni 5.4 ijayo. Jua ambalo ndio msingi wa mfumo huo, mfumo wake wa sasa unaelezwa kubadilika litakapotimiza miaka bilioni 10. Mabadiliko yanayotarajiwa ni jua kuacha kutoa gas yake asilia ya hydrogen kitu ambacho kitalifanya kubadilika rangi nakuwa jekundu ( kwa sasa jua ni jeupe na halijawahi kufanya mabadiliko yoyote yale ), kuongezeka ukubwa maradufu na kushindwa tena kutoa usumaku wa asili ambao unaziongoza Sayari ambazo unalizinguka na mwisho wa siku kuvunjika kwa mfumo huo na jua kugeuka kuingia kwenye kundi la nyota zinazojulikana kama RED GIANT.
Asanteni.
Samuel Samuel
Karibu kwa maoni na ushauri.
LikeShow more reactions
Comment

No comments: