Watanzania
13 wamefariki na wengine nane kujeruhiwa katika ajali iliyotokea usiku
wa kuamkia leo katika eneo la biashara Lubanda takribani kilomita 80
kufika kituo cha polisi cha Fika salama karibu na Mto Katonga wilaya ya
Mpigi huko Kampala, Uganda.
Ajali
hiyo imehusisha gari aina ya fuso yenye namba za usajili UAH 970P na
coaster yenye namba T540 DLC waliokuwa wakitumia watu hao wakiwemo
watanzania ambao inasemekana walikuwa wakitoka kwenye harusi ya binti
wa Dkt. Annette Ibingira ambaye ni mke wa mhazini wa shule ya Wazazi ya
Kampala nchini Uganda Dkt. Ibingira.
Majeruhi
wa ajali hiyo wamepelekwa katika hospitali ya Nkozi pamoja na Double
Cure Clinic zilizopo nchini Uganda huku miili ya watu waliopoteza maisha
katika ajali hiyo imepelekwa hospitali ya Gombe kwa ajili ya kufanyiwa
uchunguzi nchini humo.
No comments:
Post a Comment