Kamanda
wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam Lazaro Mambosasa, amesema
watu waliokamatwa na polisi hapo jana kwa kufanya mkusanyiko usio rasmi,
walishaonywa kutofanya hivyo lakini hawakujali hivyo sheria itachukua
mkondo wake dhidi yao.
Kamanda
Mambosasa amesema hayo leo na kusema kitendo cha kufanya mkusanyiko
usio rasmi ni kuvunja sheria, hivyo lazima watafikishwa Mahakamani
kujibu shtaka lao, huku akikanusha kuwakamata watu hao kwa kutokana na
kuvaa t-shirt zilizoandikwa 'pray for Tundu Lissu'.
"Kwanza
ifahamike hatujawakamata kwa kosa la kuvaa tshirt, zile ni nguo kama
nguo nyingine wanavyovaa mashabiki wa Simba na Yanga, hawa walichofanya
mpaka wakamatwe ni kufanya mkusanyiko usio rasmi na kibaya zaidi
tulishawaeleza, na wenyewe walipoona polisi wanakuja wakaanza kutukimbia
kwamba walijua wamefanya nini", amesema Kamanda Mambosasa.
Kamanda
Mambosasa ameendelea kwa kusema jeshi la polisi linaendelea kuwahoji
watu hao na kisha kupelekwa Mahakamani kusomewa mashtaka yao ili sheria
ifanye kazi yake.
No comments:
Post a Comment