Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemtaka Mkuu wa Magereza nchini kujieleza
endapo mshtakiwa Harbinder Sethi, hatapelekwa kutibiwa katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Uamuzi
huo umefikiwa na Hakimu Mkazi Mkuu, wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi
leo, baada ya Wakili wa Sethi, Joseph Makandege kuiomba mahakama leo
kufuta kesi hiyo inayomkabili mteja wake na James Rugemarila, ili Sethi
apate nafasi ya kutibiwa.
“Naomba
mshtakiwa huyo apelekwe Muhimbili na endapo hadi tarehe ya kesi
itakapotajwa kama hajapekewa Mkuu wa Magereza aje kujieleza kwa nini
hawajampeleka,” amesema Hakimu Shaidi.
Katika
maombi yake hayo, Makandege anadai mashtaka hayo yamefunguliwa kwa hila
na upande wa Jamhuri umekaidi amri ya mahakama kwa kushindwa kumpeleka
mteja wake Muhimbili, kama mahakama ilivyoamuru zaidi ya mara tatu.
Makandege
pia amedai kushindwa kumpeleka hospitali mteja wake kunahatarisha afya
yake kwani akikosa kupata matibabu sahihi anaweza kupoteza maisha
kutokana na maputo aliyowekewa tumboni.
Sethi na Rugemarila wanakabiliwa na mashtaka 12 yakiwamo ya kutakatisha fedha
No comments:
Post a Comment