Polisi wa wa Afrika kusini wamefanya msako kwa siku ya pili katika mji wa Alexandra ili kuwasaka wale wanotekelza ghasia dhidi ya wahamiaji
Vikosi vya usalama nchini Afrika kusini vimefanya uvamizi kwa usiku wa pili mjini Johannesburg huku serikali ikijaribu kumaliza ghasia dhidi ya wahamiaji kutoka mataifa mengine ya Afrika .
Mara hii vikosi vya usalama vililenga makazi ya wanaume katika kitongoji cha mji wa Johanesburg cha Alexandra ambako mashambulizi kadhaa dhidi ya wahamiaji yalifanyika katika wiki za hivi karibuni.
Maandamano makubwa ya kudai hatua zichukuliwe kukabiliana na ubaguzi yanatarajiwa kufanyika mjini Johannesburg baadaye hii leo .
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma amesema kuwa ameazimia kushughulikia masuala muhimu yanayosababisha chuki baina ya raia wa nchi yake na wahamiaji.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment